News

Hatimae Alikiba akabidhiwa tuzo yake ya MTV EMA

By  | 

Ali Kiba aka king Kiba kakabidhiwa tuzo yake aloshinda ya MTV EMA

“I would like to thank God for the continuous blessings, my family, my management and the fans. I love you all endlessly !!#MTVEMABestAfricanAct #KingKiba,” ameandika Kiba baada ya kupewa tuzo hiyo.

Tuzo ya Alikiba ilikuwa na utata badaa ya awali kupewa Wizkid ambaye baadae mashabiki walivalia njuga tuzo hiyo mpaka ikarudishwa kwa Ali Kiba , kura zilionesha kuwa ni Alikiba ndiye aliyeshinda.
Lakini baada ya MTV EMA kujua makosa yao, waliamua kumpokonya tuzo ya Best African Act Wizkid na kumpa Alikiba ambaye alistahili kushinda.

Baada ya taarifa rasmi ya MTV EMA, kuhusu ushindi wake, Alikiba aliandika:

Namshukuru MUNGU Na Shukrani kwa MTV kwa heshima hii, nina furaha sana kwa ushindi huu, ni heshima kwangu na nchi yangu Tanzania 🇹🇿

pamoja na East Africa nzima kiujumla. Shukrani sana kwa familia yangu, management yangu na mashabiki zangu wote – nawapenda sana #bloodfanswaalikiba #Kajiandae #KingKiba

Aliongeza,

“Ningependa pia kuchukua nafasi hii kushukuru vyombo vya habari vyote, watangazaji, waandishi na wadau wote wa sanaa kiujumla kwa kunisapoti katika kazi zangu.

Lastly, nawashukuru wasanii wenzangu wote mlionipa ushirikiano na kuthamini kipaji changu kwa kuniombea kura zilizonipa ushindi. Ushindi wangu ni ushindi wa sanaa yetu sote. Proudly Tanzanian 🇹🇿
MUNGU awabariki sana. #TupoPamoja #Kajiandae #KingKiba

Namshukuru MUNGU Na Shukrani kwa MTV kwa heshima hii, nina furaha sana kwa ushindi huu, ni heshima kwangu na nchi yangu Tanzania 🇹🇿 pamoja na East Africa nzima kiujumla. Shukrani sana kwa familia yangu, management yangu na mashabiki zangu wote – nawapenda sana#bloodfanswaalikiba #Kajiandae#KingKiba”

0
HeartHeart
0
HahaHaha
0
LoveLove
0
WowWow
Voted Thanks!

Leave a Reply

%d bloggers like this: