AFRIKA MASHARIKI YATIKISWA NA MAKEKE

Msanii wa mitindo kutoka Tanzania JOCKTAN  MAKEKE jana kafanya maajabu tena kwenye jukwaa la mitindo la AFRICA FASHION WEEK 2016 ambalo limefanyika Nairobi katika hotel ya boma na limehusisha nchi zote za jumuiya ya AFRIKA MASHARIKI , Tanzania, Kenya , Uganda, Rwanda , Burundi na Sudani kusini .Kama kawaida ya makeke kaendelea kukimbiza na collection yake ya THE AFRICAN BEAUTY IN THE DARKNESS (TABID) au kwa kiswahili ni uzuri wa Afrika gizani , makeke amesema kuwa ametumia giza kuwakilisha utamaduni wa kimagharibi ambao kwa sasa umekuwa umeivamia Afrika kwa kasi ya ajabu kitu ambacho kinafanya waafrika wengi kujisahau na
kujiona tayari wamekuwa wa marekani, lakini licha ya kuwepo kwa giza nene bado Afrika ina shine kwani kuna tamaduni ambazo zinafaa kuigwa zaidi na mataifa mengine, Runway iliambatana na wimbo wa SIZONJE wa Mrisho Mpoto ili kukamilisha ladha ya KIAFRIKA,  Makeke aliongozana na wanamitindo wawili, Paulina mgeni na Violet Peter ambao pia wameiwakilisha Tanzania vyema mno na kukutana na fursa mbalimbali kwenye agency za wanamitindo kubwa  Afrika mashariki, katika kufanikisha hilo MAKEKE katoa shukrani za dhati kwa 8020 FASHION , BONGO 5, SUPER NEWS na watanzania wote walioonyesha support ya nguvu…★★★

IMG-20160327-WA0040

 

IMG-20160327-WA0044

IMG-20160327-WA0045

IMG-20160327-WA0049

IMG-20160327-WA0051

IMG-20160327-WA0052

IMG-20160327-WA0054

IMG-20160327-WA0056

Related Posts

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.