Airtel na UNESCO wazindua radio ya kwanza Uvinza Kigoma

•      Ni radio ya kwanza kusikika Uvinza
•      Wakazi wa Uvinza na vijiji vya jirani sasa kupata taarifa na habaza
za ndani nan je ya nchi
Kigoma Uvinza Jumanne 30 Septemba 2014,  Kampuni ya simu za mkononi ya
Airte kwa kushirikiana na  UNESCO  leo imewawezasha wakazi wa Uvinza
kupata taarifa za kimaendeleo na habari  za ndani na nje ya nchi
kufatia uzinduzi wa radio jamii Uvinza Kigoma
Akiongea wakati wa uzinduzi wa radio hiyo ulifanyika mkoani Kigoma
mwisho mwa wiki, Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi
alisema” Tunayo furaha kuwa mstari wa mbele katika kuleta mapinduzi ya
mawasiliano kwa kushirikiana na UNESCO kupitia mradi huu wa Radio
jamii na kuwawezesha wakazi wa uvinza kupata mawasiliano ya radio.
Radio jamiii tunayozindua  leo itawawezesha wakazi zaidi ya 400,000
wanaoishi Uvinza na vijiji vya jirani kuweza kupata habari na taarifa
ya yale yanayotokea Tanzania na duniani kwa ujumla
Tunaamini kwa kupitia mradi huu wa radio jamii tutawawezesha jamii
zinazoishi pembezoni mwa nchi ambazo hazijafikiwa na mawasiliano ya
radio kupata habari na taarifa muhimu zitazowapa  kupata elimu juu ya
mswala yatakayowasaidia jamii katika uwekezaji endelevu. Radio hii
jamii itakuwa ni chachu katika kuwawezesha jamii kuwa na uhuru wa
kutoa maoni yao, kuboresha  mambo yakijamii, na mwisho kubadili maisha
ya wakazi wa uvinza kwa ujumla . aliongeza Bayumi
Ushirikiano huu wa kipekee na wenzetu wa UNESCO umelenga katika
kushughulikia changamoto zinazozinguka jamii ikiwa ni pamoja kuboresha
utawala bora, kuondoa umasikini, kuondoa ujiga, kuhamasisha elimu wa
mtoto wa kike  huku tukihakikisha mradi huu unakuwa chachu na njia kuu
ya kuleta mafanikio ya kiuchumi na kijamii katika wilaya ya Uvinza
Kwa kuongezea  Misimamizi wa Mradi wa habari na mawasiliano wa UNESCO
Dar es saalam Bwana Yusuph Al Amin alisema” ushirikiano wetu na Airtel
umekuwa wa mafanikio makubwa  mpaka sasa tumeweza kuwafikia watanzania
zaidi ya million 16 kwa kupitia radio hizi zilizoko katika maeneo
mbalimbali ya nchi. Na Radio hii ya Uvinza inafanya jumla ya radio 4
ambazo tumeshazizindua rasmi kupitia ushirikiano huu.
Tumeweza kuweka vifaa vya matangazo na vya kutengeneza vipindi vya
radio vya kisasa vyenye technologia bora na kuwapatia wafanyakazi
katika radio hizi mafunzo pamoja na vitendea kazi vitakavyowawezesha
kutoa huduma bora kwa jamiii. Sambamba na hilo vipi vinavyorusha
katika radio hizi ni mahususi na vimelengwa kutoa elimu kutatua
changamoto katika jamii husika ambapo radio hizi zinarusha matangazo
yake , hivyo tunachukua nafasi hii kuhamasisha jamii na wakati wa
maeneo hayo kutumia radio hizi kwa ajili ya kuleta ufanisi katika
jamii na maendeleo katika uchumi wao kwa ujumla aliongeza Al- Amin

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio  Nuru Kalufya
alitoa pongezi zake kwa Airtel na UNESCO kwa msaada walioutoaka kwa
wakazi wa Uvinza na kusema “naamini wakazi wa uvinza na maeneo ya
jirani sasa watafaidika na kufurahia vipindi mahiri zitakavyorusha
kupitia radio hii zinavyolenga kuzungumzia changamoto mbalimbali na
namna ya kuvitatua huku zikionyesha maeneo yenye fulsa za uwekezaji
ili kuboresha maisha ya wanauvinza. Changamoto tuliyonayo ni kuona
jinsi gani tunavyoweza kufikisha mawasiliano ya radio katika maeneo
mengi zaidi ya mkoa wa kigoma ambayo mpaka sasa hayajapata mawasiliano
ya radio.

DSC_0085 DSC_0120 DSC_0206

Related Posts

Leave a Reply