Diamond Platnumz kufunga ndoa mwaka huu ,Je nani anafunga nae ndoa??

Jana ilikua kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani,Diamond Platnumz hakua nyuma kumu wish Mama yake na wanawake wote ulimwenguni.

Kati ya mengi aliyo andika moja wapo ni yeye kumshukuru mama yake mzazi na kusitika pia kua amekua akitunkanwa sana kwa ajili yake but kuuuuubwa kuliko ni yeye kumuahidi mama yake kwamba mwaka huu anafunga ndoa.Ni jambo la kheri sana hili ila watu wengi mmoja wapo mimi tumekua tukijiuliza nani huyo anafunga naye ndoa???

Maana ameachana na Zari wakati wa valentines actually aliachwa,Wema kasema hayupo nae ,Hamisa pia hawako vizuri so who is the mysterious woman ambaye ataolewa na Diamond???

Mana kunakuwaga na rumors but this time holaaa ,tufanyaje???let’s wait and see.

Alipost hii picha kwa page yake ya insta na kuandika hivi

Happy Women’s day Mama na wanawake wote Ulimwenguni… Nashkuru sana kwa kunizaa na kunilea…Wewe ni Mboni na Nguzo ya Maisha yangu mama…Licha ya shida na Mateso uliyoyapata kwenye kunizaa na kunilea, lakini hata sasa ambapo ulitakiwa walau Upumzike nimekuwa nikikukosea kwa kukuingiza hata kwenye Matatizo Yasiyokuhusu…Wanakutukana, wanakukebehi na kukutupia kila neno lililo baya, yote kwa sababu yangu mimi, lakini sikuzote umekuwa mwenye kunisamehe, kunipenda na Kunithamini…..Nakupenda sana Mama, Na nisameh kwa yote nilokukosea… Inshaalah, Mwenyez Mungu anibariki Mwaka huu Mwanao nifanikishe Ndoa yangu na kukupa Furaha ya Milele ambayo siku zote umekuwa Ukiitaka….. @mama_dangote

Related Posts

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.