PSPF & FMF WAKABIDHI VIFAA LINDI

Mfuko wa Pensheni PSPF kwa kushirikiana na Flaviana Matata Foundation wametembelea na kutoa misaada ya
vifaa vya shule kwa wanafunzi wa shule za msingi waishio katika mazingira magumu katika wilaya za Lindi na
Nachingwea mkoani Lindi. Ziara hii imelenga zaidi kuinua kiwango cha elimu nchini Tanzania kwa kusambaza
vifaa vya shule kwa wanafunzi wenye uhitaji. Pamoja na hayo ziara hiyo pia ilikuwa na lengo la kuainisha
changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini Tanzania.
Msafara huo uliongozwa na Flaviana Matata, mwanamitindo mashuhuri wa Kitanzannia anayefanya kazi zake
nchini Marekani na muasisi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Flaviana Matata Foundation kwa pamoja na Meneja
wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Costantina Martin. Ziara hiyo ya siku
moja mkoani Lindi ilijumuisha Shule za Msingi Mtua na Chemchem za Wilayani Nachingwea na Shule za Msingi
Mnengulo na Litingi za wilayani Lindi ambapo jumla ya watoto 700 walipatiwa “Stationery Kits” zilizojumuisha
madaftari kumi na mbili (12), kalamu za wino tatu (3), kalamu za risasi mbili (2), Kompasi (mkebe) mmoja (1),
Ufutio mmoja (1) na begi la shule moja (1). Vifaa hivyo vinatarajiwa kuwasaidia wanafunzi hao katika muhula
mmoja wa masomo.
Lengo kuu la msaada huu uliotolewa kwa pamoja kati ya Mfuko wa Pensheni PSPF na Taasisi isiyo ya kiserikali
ya Flaviana Matata Foundation ni katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kwamba kila mtoto
nchini Tanzania anapata elimu akiwa na vifaa muhimu vinavyohitajika. Pamoja na hilo ziara ilikuwa na lengo la
kuainisha changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini Tanzania na kutoa hamasa kwa wadau mbalimbali
kushiriki katika harakati za kuikwamua elimu kwa kuchangia katika maendeleo yake kwa namna moja au
nyengine.
Akizungumza katika ziara hiyo muasisi wa Flaviana Matata Foundation alielezwa jinsi alivyosikitishwa na jinsi
ambavyo watoto wa Kitanzania wanapata elimu katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na ukosekanaji wa
madarasa ya kudumu, watoto kusomea chini ya miti, uhaba wa vyoo vya kisasa kiasi cha kuhatarisha maisha ya
wanafunzi kutokana na magonjwa ya milipuko, uhaba wa walimu, uhaba wa nyumba za walimu na vifaa vya
kufundishia. Flaviana Matata alitoa ahadi kwamba atapambana kadri ya uwezo wake kwa kuwashirikisha
wadau mbalimbali kuhakikisha sekta ya elimu nchini inaboreshwa.

Hii ni mara ya pili kwa Mfuko wa Pensheni PSPF kushirikiana na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation katika
kutoa misaada yenye malengo ya kuboresha sekta ya elimu nchini Tanzania. Katika awamu ya kwanza jumla ya
wanafunzi 1500 waishio katika mazingira magumu walifaidika na msaada huo katika mikoa ya Pwani na
Shinyanga. “Tunatarajia kuwafikia jumla ya watoto 3000 waishio katika mazingira magumu nchini Tanzania
hususani katika wilaya za Tunduru na Monduli tutakapokuwa tunamaliza awamu ya pili ya usambazaji wa
misaada hii ya PSPF na FMF” alisisitiza Meneja Masoko wa PSPF Bi. Costantina Martin.
Katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuinua kiwango cha elimu nchini, Taasisi ya Flaviana Matata
imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali na watu binafsi katika harakati za kuinua kiwango cha elimu nchini.

Flaviana matata

2G2A8088

Flaviana Matata ameongozana na Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin  pamoja na wafanyakazi wa PSPF katika zoezi la kukabidhi vifaa hivyo.  Martin

2G2A8156 2G2A8174 2G2A8196 2G2A8234 2G2A8248 2G2A8279 2G2A8299

IMG-20140811-WA0044 IMG-20140811-WA0023 IMG-20140811-WA0029

 

USISAHAU KUNIFOLLOW INSTAGRAM @8020FASHIONS ILI UWEZE PATA UPDATE SAMBAMBA NA KUDISCUSS HAPO KWA PAPO  YANAYOJIRI DUNIANI NAPIA HAPO JUU KULIA WEKA EMAIL YAKO ILI UJISAJILI TUWE TUNAKUTUMIA YANAYOJIRI BLOGUNI HATA KAMA HUJAFUNGUA BLOG, BILA KUSAHAU PERUZI BLOG KUPITIA SIMU YAKO

Related Posts

1 Comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.