Flaviana Matata Foundation yatoa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi 290 pamoja na vifaa vya kufundishia kwa walimu wa Shule ya Msingi Msinune

Leo tumetoa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi 290 pamoja na vifaa vya kufundishia kwa walimu wa Shule ya Msingi Msinune .

Flaviana Matata Foundation mbali na kusomesha watoto wa kike, tumekuwa tukitoa vifaa vya kujifunzia (learning tools) kwa wanafunzi wa shule mbalimbali nchini kwa miaka minne sasa; Shule ya Msingi Msinune ni mojawapo kati ya shule za mwanzo na tumeendelea kufanya nao kazi kwa ukaribu ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kama sehemu ya kutatua chagamoto zinazoikabili shule ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora bila kuwasahau walimu maana bila wao hatuwezi kufanikisha malengo yetu.

 

 

 

Related Posts

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.