”Instagram ndio sehemu pekee ambayo watu wanakupangia namna sahihi ya kuishi ” Zamaradi Mketema

Wakati Salma Msangi akipigania watu wasiandike waraka ila nafikiri ni kwenye mambo ya wishes za Birthday tu,Zamaradi yeye anaendelea kuandika waraka sababu anapenda kuandika na wengine tunapenda mawazo yake na busara zake anazoandika.

Jana aka amua kuwashushia maneno watu wanaotumia instagram kuanza kupangia watu maisha,marafiki wa kuwa nao ,marafiki wakutokua nao nk.

Instagram ndio sehemu pekee ambayo watu wanakupangia namna sahihi ya kuishi (kulingana na maono yao) bila kujali wala kujua hali yako

Sehemu pekee utakayochaguliwa yupi anafaa na yupi hafai

Sehemu pekee utakayohojiwa na kuhukumiwa kwa maisha yako binafsi kutokana na kuishi maisha yako ya ukweli

Sehemu pekee utakayooneshwa yupi wa kuwa nae na yupi wa kumuacha

Lakini cha kuchekesha ndio sehemu pekee utakayochukiwa sio kwa UBAYA WAKO ila kutokana na kuelewana na mtu wasiempenda wao.

Na zaidi ndio sehemu pekee utakayopendwa pia sio kwa UZURI WAKO ila kufuatana na wanaomtaka wao’

Kiufupi ni Sehemu pekee ambayo maisha yako yako yanapangwa na wengine bila haya wala aibu

Sehemu pekee wanayotukuza UNAFKI na kuubeza UKWELI

Kumbuka tu ukweli wa maisha yako ni vile unavyoishi ndani bila picha wala video hivyo ukitaka kufanya kama muda wote unaonekana utaishia njiani kwenye mengi na utapoteza wengi wa ukweli.

Maana hii ni Sehemu pekee ambayo KAMA HUNA MSIMAMO utaishia kuwa mtumwa wa fikra na mawazo kwa kufatisha watu ambao hawajawahi kufanya wanayokuamrisha

ISHI MAISHA YAKO, faana na anaekufaa, penda anaekupenda, usimtenge mtu wako kwa kuogopa waja, wala usiwe mdananda wa wengine kwa kufurahisha usiowajua

Maisha yako HAYATAPINDA kutokana na maneno ya watu ila yale uyatendayo juu ya maisha yako, na wala usitegemee YATANYOOKA kwa kupigiwa makofi na usiowajua ikiwa wewe unayoyafanya ni tofauti (huna juhudi binafsi). Kuwa na msimamo juu ya maisha yako, dont take INSTAGRAM life too serious. Wengi katika wabezaji ya kwao yamekwama njiani. – ZAMARADI

Related Posts

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.