#instapreneurTZ :CHANGAMOTO ZA KUKOPA NA KURUDISHA MKOPO KWA MJASIRIAMALI

Juzi nilipost post kwa instagram yangu Swali nikiuliza  ”

Nini Kikwazo wengi wa wanajasiriamali wanashindwa kukopesheka na  wanaokopesheka marejesho yana zasumbua mno

Majibu nilopata Baadhi ingia kwenye LINK hii usome huko Instagram  lakini mimi nikatoka na jibu kuwa:

Wengi wa wajasiriamali wanaingia kwenye ujasiriamali  Kuonekana kama nae anafanya kitu kwenye jamii  AU kusaka pesa ya kusogeza maisha yani kupata kitu cha kumfanya mkono uende kinywani ndio maana kuna biashara ya msimu

mfano atokee mtu aseme “kufuga kuku kunalipa kunalipa ” basi mtaa mzima kama sio wilaya itahamia kufuga kuku, Hapa majuzi sijui alitokea nani yarabi na mradi wake wa KWALE

Wilaya mzima ya Kinondoni kama sio kama sio mkoa (nazungumzia Kinondoni sababu ndio wilaya nayoishi na nilikua nakutana nayo hayo mayai ) unaenda gengeni unaambiwa nunua dada haya mayai mazuri kwa watoto na familia yana vitamini zoote ……sasa wengine wakujiulizaga twajiuliza izo vitaminiiii zooote zilizopatikana kwale leo hii na sikuwahi kuzipata si ningekuwa nishajifia …….. kuja kugundua ni kiingiacho mjini Unaelewa ndo wale wale wazee wa kutrendisha Biashara

Huo ulikuwa ni mfano tu lakini kuna biashara nyingi saana zinaanzishwa kwa mkumbo  na ndio haswaa tatizo linalopelekea Mjasiriamali kutofahamu biashara anayoifanya vyema na nani mteja wake na atauza wapi  as eneo lipi itamgharimu nini nk

Hivyo basi na mabank wanahitaji wateja akienda kukumbana na mfanyabiashara yule ndo hapo tatizo linaibuka ni kweli ataweza Kidhi kigezo cha mkopo  kupata mkopo baada ya kumshawishi mume au bwana aweke gari au hata amdhamini kwenye hati ya nyumba ( tatizo si hati tu ) bada ya hapo sasa sababu ile biashara haijasimama anaeiendesha haijui ndo hapo Mtihani unapoanza

Hapo sijamzunguzia Mwanadada Fatuma aliyepata bahati ya kupata Danga akasafiri nalo kikazi nchini China au Dubai akapita madukani akaona hivi vitu si ndio wanavyouzaga kariakooo na Maduka ya Sinza kitop huku 3000 kule twauziwa 20,000 basi Bidada atajibebisha atapesa dola 500 yake atafunga begi zake 2  nae akija akapata Frem ya 50,000 kapewa laki 300,000 ya miezi 6 basi nae atakuwa mmiliki wa Fettylicios Boutique na vyeo kibao vya Boss Lady na CEO instagram. InstapreneurTanzania Mpo ?

Ndo hapo akakutana na muajiriwa mpya wa Bank  Mpya aliyepewa target ya mwezi kuleta  wateja 10 wa kukopa akamshawishi kuwa utapata mkopo tu si una duka hapa TIN ya biashara ni bure leseni 80,000 na unayo Gari tutaweka kama Dhamana  (kumbuka gari alihongwa na Boyfriend wake alooa ambaye alimpa kama KIFUTA MAHUSIANO )  fungua akaunt na sisi uwe unaweka pesa kisha utapata mkopo

Sasa niambie Dada Fatuma atakuwa anajua biashara kweli je mkopo atarudishaje , lini tena Danga la Dubai litapata trip yakumbeba yeye ili akachukue mzigo kumbuka Fatuma sio kwamba atakuwa anakaa dukani ataajiri mdada wa dukani wa kumuita Madam  na kumshushia mizigo nae anahitaji mshahara

Kwastyle hii Dada Fatuma atarejesha kweli deni wengi waliishindwa biashara duka lafungwa Bank mnabaki na kadi na mkijitahidi saka gari utakuta liko police lilishagongwa dada Fatuma alopata ajali sitaki  kuwaza na fuatilia kama aliwahi kukimbia  asishtakiwe kwa kuendesha gari akiwa amelewa au yuko hospitali katundikiwa.

Na kwa kugundua haya sasa ndio Maana NMB BANK ikaanzisha akaunt ya FANIKIWA AKAUNTI ambapo ukishafungua akaunt na bank unapata nafasi ya kuingia kwa BUSINESS CLUB ambapo ndani yake kunafundishwa masuala tofauti jinsi ya kuendesha biashara , mikopo NK

UKIPENDA JIUNGA NA FAMILIA YETU  tembelea  watawi yetu zaidi ya 200 nchi nzima / mawakala zaidi ya 400 na ATM zipatazo 800 #NMBKARIBUYAKO

1 Comment

  1. Thank you Shamim. But would suggest pia na way forward apart tu from kujiunga na account ya Fanikiwa NMB je sisi kama Instaprenuers how do we jikwamua from haya majanga ya kupata mkopo na kushindwa kulipa sababu zikiwepo nyingi au ata experience za wengine za namna ya kujikwamua from madeni au namna gani mtu afanye ili aweze kumake profit but as well kufanya marejesho na kufanya maamuzi sahihi.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.