Je Umewahi Kusalitiwa Na Best Friend Wako? Ulijifunza Nini?

“Leo tuongelee ushosti jamani, mie ni muhanga wa kusalitiwa na best friend zangu sio mara moja wala sio mara mbili. nikajikuta siamini tena rafiki kabisa na mpaka sasa sina rafiki wa kusema tumeshibana. mashosti tunakutana tu kwenye vikundi tuna have fun basi. simpi mtu nafasi ya kunijua sana undani.
Kabla sijaolewa nilikua na shost namuambia kila kitu changu. kumbe yy anamwambia boyfriend wangu kila kitu. nikashangaa jamaa kakata kamba ghafla na sikujua. nikapata mwingine nikajua huyu ndio tunaoana. nikawa namueleza shost mipango yangu yote! hee akamtafuta jamaa akawa anampa maneno weee mpaka jamaa nae akanitema. Mungu akanisaidia nikapata mwingine nikajifunza kuwa msiri, yule BF aliyepita alivyoona naolewa ndio akaja kuniambia shoga ako ndio alitugombanisha! baadae tena nikakutana na yule mwingine akanieleza hicho hicho! nilijuta!
hivi mwanamke ukimuharibia mwenzio unafaidi nini? hebu tujadili maana haya yanafanyika maofisini, kwenye biashara kila mahali, shida nini? pole kwa gazeti”

87464562

New topic kwa 8020Forums tukidiscuss pamoja na mashosti ndio hiyo. Ni kweli hawa mashosti tulionao wankua wazuri machoni tu lakini ukiwa haupo huwezi kuamini ni mambo gani anasema kuhusu wewe.. kuna wale  nadhani wote tunaqwajua watu kama hao.

Zama humu www.8020forums.com na wewe ujiunge nasi kwenye talks zetu na mashosti, Feel free kwasababu unaweza kujiregister anonymously na mtu yeyote asikujue.

Feel free pia kuanzisha mada yako au ahata kuuliza maswali. Mashosti tupo tutakujibu na tutaendelea kudiscuss different topics.

Related Posts

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.