Kina Mamam Hivi ni Baadhi ya Vitu ukivifanya vinakupa Matumizi Mapya ,Nakujuza

Hii post niliiona huko Facebook kwenye group la Wanawake mahiri,mashujaa na wanaojua mambo mengi ,huwa jina lingine ni JESHI KUBWA LA MAMA ,humo hakishindikani kitu,basi nilipo ona hii post kwakweli nilisema baadhi ya vitu lazima niweze kuvi share huko kwa Wadada na kina Mama wenzangu sababu knowledge is power.

Wanawake walitaja vitu vingi sana na nita share tu baadhi vingine mkacheki huko,na naomba nitoe onyo sio vitu vyote vilivyotajwa nimeshawahi kujaribu ni elimu tu tunapeane kazi kwako kwenda kujaribu na kuleta mrejesho.

1.NIMEKOSA MAJANI YA CHAI, NITAUNGUZA SUKARI, KISHA NITAWEKA MAJI, TAYARI NIMEPATA CHAI, ..

2.NITAITUNZA STEEL WIRE NDANI YA MAJI, NIKAWEZA ITUMIA KWA KIPINDI KIREFU

3.HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIEKUNYWA MAFUTA YATAA ,SAGA MKAA KISHA KOROGA KTK KIKOMBE MPE ANYWE

4.MTOTO MCHANGA AKIKOSA CHOO KWA SIKU KADHAA CHUKUA SABUNI YA KIPANDE NA PAMBA YA KUTOLEA UCHAFU MASIKIONI KISHA ITIE MAJI ILE PAMBA NA SABUNI ITIE MAJI KISHA CHUKUA PAMBA ISUGUE KWENYE SABUNI ILI IKOLEE SABUNI KISHA MPITISHIE HUKO SEHEM YA HAJA KUBWA DK TU ATAANZA KUJINYONGA NA KUTOA CHOO KINGII,ILA ANGALIA PAMBA ISIBAKI NDANI

5.ILI PILAU LAKO.LIWE NA TEST HAKIKISHA HUWEKI VITUNGUU SAUM KWENYE MAFUTA ,VITIE BAADA YA VITUNGUU MAJI KIWA BROWN KISHACWEKA SUPU NA VIUNGO VYA UNGA THEN VITUNGUU SAUM ,PILAU LITANUKIA NA KIWA NA TEST NZURIII

6.Kama upo safarini au upo maeneo ambayo umezidiwa na haja kubwa hamna haja ya kumsumbua dereva!!! 7.Unachukua mate unapaka kwenye kitovu kwisha habari yake ngoma mpaka ufike sehemu usikaaaa!!!

8.nitatumia bicarbonate of soda na limao kuondoa weusi kwapani

9.Karai/ sufuria yako ina kutu na hata kwa steelwire haitoki….. bandika sufuria/karai lako jikoni likianza kushika moto sugua na kipande cha limao likiwa hapo hapo jikoni. Kutu yote inatoka linakua safi.. then unaosha na dodoki

10.Km upo safarini na ukapata tumbo la kuhara kunywa Maji baridi sana kiasi tu na tumbo litaacha koz utagandisha tena mafuta yanayovuruga tumbo na utakua salama ila ukifika kunywa chai moto kayatoe tu.

11.Vikombe vya udongo vilivyoweka rangi ya chai hadi unaona aibu kumkaribisha mumeo chai…vioshe kwa tumia majivu au stilwaya utavipenda vitakavyong’aa/Vim na still wire ndivyo natumiaga

12.Chungu ama sufuria jaza majivu unakuwa unafukia moto mle kwny majivu haki,Kuomba moto kwa jirani au kuwasha kwa mafuta ya taa utayasikia tuu kwa watu.

13.Ukichemsha maziwa ili yasimwagike weka kisosa cha chai ndani ya sufuria /kijiko au uma pia

14.Ukipika wali ama mboga mfano wa maharage kwa bahati mbaya ukaunguza,ucmwage badili sifuria na kimenye kitunguu then kitie bila kukikata,harufu haitoi na wala radha ya kungua hitoisikia.

15.Ukitaka Kufua taulo yako ing”ae vizuri,fulia maji ya moto sana itakua supa

16.Ukipika mchuzi wa nyama ukawa mwepesi sagaa kiazi mviringo juu yake utapata rojo zito.
Au koroga ngano kidogo weka, ukikosa ngano tumia sembe kidogoo korogo chuzi zitoooooo

17.Ukikaangia mafuta samaki ukimaliza kuwatoa samaki kamulia ndimu au limao shombo na harufu yote utatoka, mafuta yatafaa kwa matumizi mengine

18.Ukikosa mkaa na una hamu ya maharagwe! Chemsha maji yachemke vizuri weka maharagwe kwenye themos tia Yale maji yaliyochemka funika vizuri! Usiku asubui yamekwiva vizuri kabisa yamoto!

19.Ukichemsha mayai na hutaki yapasuke weka chumvi ichemkie

20.Friji ikitoa harufu weka kaa ndani ama pangusa na bicarbonate soda

21.Pasi kama imeshika nguo na kuungua paka Colgate upanguse itaondosha ule weusi
Ukikaanga vitunguu vya biriani mwagia chumvi vitakuwa crunch

22.Maharage kuiva fasta yachambue safi chukua sufuri yako weka jikon yakaange kama karanga hadi yawe kama yanabadilika then yaoshe bandika jikon yan mapema sanaa!!

23.Ukiwa na ukoko Sugu nyweleni Au mba jisugulie Limau acha nusu saa osha
Au tangawiz, Limau, na mtindi changanya upake kichwani

24.Mikono migumu Chkua olive oil nasukari jisugulie Kila Sku Ukimaliza pirika zako baada hapo nawa kwa maji ya uvuguvugu na paka Vaseline

25.Ukizidisha chumvi kwenye wali menya kiazi mbatata tumbukiza kati kati ya sufuria ya wali chumvi itapungua.

26.Ukiunguza wali kata kitunguu maji weka kwenye wali harufu ya kuungua itapotea.
26.Ukizidisha maji kwenye mchuzi kwangu kiazi mbatata na chuzi litakuwa shatashata
28.Km una fungus sugu miguu chukua hina ya majani ikoroge na chai kidogo iwe nzito pakaa palipo athirika vaa soksi hata siku nzima fungus itakuwa historia.

29.Sink Chafu lilofubaa jikoni Chkua baking soda na siki ya apple roweka Hadi asubuh sugua linakua km jipya.

30.Mfereji Au kitu chchote kilofanya rust roweka Au sugulia na Coca-Cola kitang’aa km kipya.

31.Sisimizi Sugu wanokaa jikoni eka pilipili ya unga watahama

32.Kikohozi kikavuu tafuna majani Ya mbaazi na magadi. Ili mbaazi zisigongwe na wadudu chemsha MAJI yskichemka zitose zitoe anika hagusi miaka.

33.Kiatu kikibana chonga kiaz mbatata tumbuliza kilale humohumo kikaushe kiatu kivae kinatanuka.

34.Jikoni kukifanya vile vidudu vinavyo letwa na matunda weka vinegar kwenye sahali uweke karibu na ulipo weka matunda ama mboga.

35. Unataka kufanya biashara ya juice na huna mtaji nenda kwa wauza mananasi kusanya maganda ya nanasi chemsha mpk maji yapungue yaache yapoe saga kwa brenda ama twanga kwa kinu chuja weka sukari juice tamu na pia dawa ya UTI na magonjwa mengi tu uza glass 500 umetoka kimaisha 😂 😂 😂 😂unqweza ongeza ladha ukipenda ya embe au nanasi

36. Ukitaka kitunguu kibadilike rang fasta unapokaanga tia chumvi

Kwa yoyote mwenye mengine yakuongelea basi usisite kutuandika kwenye commenti hapo chini 

Related Posts

1 Comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.