Kumi la mwisho katika Mwezi wa Ramadhani

ALLAHUMMA INNAK ‘AFFUWWUN TUHIBBUL ‘AFWA FA’FU ‘ANNI
O ALLAH
You Are The One Who
Pardons Greatly, And Loves
To Pardon,
So Pardon Me.
AMEEN
Kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa ramadhani dio kumi iliyoteremka Qur-an na ndilo kumi tukufu kuliko yote nalo ni kumi ambalo Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam)
alikuwa akijitahidi zaidi katika kufanya ibada kuliko makumi mengine yote.na ndilo kumi linalopatikana usiku wenye cheo usiku Wa Laylatul Qadir ambao hutarajia kuwa tarehe 21,23, 25, 27, na 29, ambapo yeyete atakaekutwa anafanya ibada ndani ya usiku huo ni sawa sawa na mtu aliye fanya ibada miezi elf takiribani miaka 89, Kutoka kwa Bibi Aysha (radhi za Allah ziwe juu yake) amesema Alikuwa Mtume swalla llahu ‘alayhi wasallam ) wakati kumi la mwisho linapoingia alikuwa akienda kukaa itikaf msikitini na, akikesha usiku kwa kufanya ibada, akiamsha familia yake na akikaza shuka yake na alikuwa akijifunga kibwebwe. (kwa maana alikuwa akijibidiisha na kufanya Ibada).”

Na katika hadithi nyengine Imepokewa kwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa) kwamba: “Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akijitahidi katika kumi la mwisho kuliko alivyojitahidi katika siku nyingine zozote Katika hadithi hapo juu tunaona wazi vipi Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam) alikuwa akiimaliza ramadhan ndani ya
kumi la mwisho. Kwanza alikuwa akiutumia usiku kwa kumuabudu Allah (subhanahu wataala). Katika nyakati zilizo bora za mja kumuabudu Allah (subhanahu wataala) basi ni nyakati za usiku.

Na nyakati hizi ndizo ambazo Allah(subhanahu wataala) ametaja utukufu wa wenye kufanya ibada nyakati hizi, sala zilizo bora baada ya faradhi ni sala za usiku na pia Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam) akizitumia nyakati hizi kwa ibada. Anasema Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam) : “Atakayesimama (Kuswali) Ramadhaan kwa imani nakutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia” (Bukhaariy na Muslim).


Pia tunafahamu kuwa kila inapofika usiku, Allah huita waja wake kama alivyosimulia swallallahu ‘alayhi wasallam , “Mola wetu huteremka mpaka wingu wa kwanza katika kila robo tatu ya usiku na husema, “Ni nani ananiita Nimuitike wito wake? Nani anayenihitaji kwa haja Nimkidhie haja yake? Nani anayenitaka msamaha Nimsamehe” Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam) alikuwa akiamsha watu wake. Na hapa tunapata mafunzo makubwa sana kuwa mtu asiwe anaamka yeye tu kufanya ibada na anawasahau watu wake. Lazima tuwahimize na watu wetu kwani baba ndio mchunga na kila mmoja atakuja kuulizwa juu ya kile alichokichunga Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam) alikuwa akikithirisha kufanya ibada katika kumi la mwisho.

Miongoni mwa ibada alizokuwa akifanya Mtume(swalla Allahu alayhi wasallam) ni kukithirisha kuswali kusoma Quraan na kufanya dhikir Imepokewa kwa Aisha (Radhiya Allaahu ‘anha) kwamba: Mtume (swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akifanya Itikaaf kila kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani Mtume (swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): anasema Atakayesimama usiku wa Laylatul- Qadr kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia” Imepokewa kutoka kwa BibiAisha (Radhiya Allahu anhaa) kwamba alisema “Ewe Mtume wa Allah je, nitakapojaaliwa kufika usiku wa Laylatul-Qadr niombe nini?” Akasema, ((Sema: Allaahumma Innaka ‘Afuwwun Tuhibbul-‘Afwa fa’afu ‘anniy – Ee Allaah Hakika Wewe Ndiye Mwenye Kusamehe Unapenda Kusamehe basi Nisamehe”(Ahmad,Ibn Majah). Tunamuomba mwenyezi mungu atujalie tuwe miongoni mwa watakaosamehewa madhambi yetu Aaameeen

Related Posts

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.