Kundi la”WAKALI SISI”latimka na Milioni 5

Hatimaye kundi la”Wakali sisi” lenye makazi yake kiwalani jijini Dar es Salaam, ambalo lilikuwa miongongoni mwa makundi matano yaliyoingia fainali za shindano la kucheza muziki maarufu kama Dance 100% linaloratibiwa na Kituo cha East Africa Television ltd  na kudhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, limeibuka mshindi katika shindano hilo lililokuwa la kukata kwa shoka kwa ushindani mkali katika Viwanja vya Don Bosco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa shindano hilo Happy Shame alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, fainali za shindano hilo ambalo safari yake ilianza Julai 19, mwaka huu kuanzia hatua ya kusaka washiriki hadi mchujo lilishirikisha makundi matano.

Shame alisema, shindano la mwaka huu lilikuwa gumu na lenye kuleta msisimko wa aina yake zaidi kuliko miaka miwili iliyopita baada ya mambo mbalimbali kuboreshwa na zaidi kiasi cha vijana kuwa wabunifu na kuona ni fursa kwao sio tu kupata fedha, pia kuendeleza vipaji vyao na kujinasua kiajira.

“Ushindani umekuwa mkubwa sana katika shindano la mwaka huu ikilinganishwa na miaka mingine kutokana na sababu mbalimbali.  Shindano pia limeanza kupata mashabiki, tunashukuru sana sapoti ya wadhamini wetu Vodacom Tanzania,” alisema.

Naye Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu,alieleza kwa  niaba ya kampuni aliridhishwa kabisa na matokeo na aliwapa pongezi kundi la wakali sisi kwa kuipuka na ushindi huo.

Nkurlu alisema  kuwa, kundi hilo lilistahili ushindi kwasababu lilikuwa makini na kufurahia kwa kile walichokuwa wanakifanya kwa moyo mkunjufu na kujitambua kana kwamba wapo kazini.

Alisema kampuni ya Vodacom inajivunia na kujisikia fahari kwa kudhamini shindano hilo kwa njia hiyo ya udhamini wakitambua umuhimu wa vijana kujiajiri kupitia vipaji vyao na kuongeza kuwa, kwa kipindi chote cha mchakato wa shindano hilo, amejifunza mengi kutoka kwa vijana hao walioshiriki katika shindano hilo kuwa ubunifu ni kitu muhimu sana.

“Vijana wameonyesha uwezo mkubwa kuanzia hatua ya mchujo hadi sasa kiasi cha kuwapa majaji wakati mgumu. Tunaamini hata baada ya fainali hizi, vijana hawa watajiendeleza zaidi kimuziki,” alisema Nkurlu.

 

Makundi matatu yaliyofanikiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali katika hatua ya fainali hiyo na vijana walikuwa wakionesha vipaji na umahiri mkubwa wa kucheza staili mbalimbali za muziki ambayo ni Wakali sisi walioibuka kidedea na kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 huku kila mshiriki katika katika kundi hilo akipatiwa simu aina ya Vodafone Smart Kicka ikiwa na muda wa maongezi wa sh. 100,000.Mshindi wa pili ni kundi la The W.T. na kuondoka na kitita cha shilingi Milioni 1 na laki 5 na mshindi wa tatu ni kundi la  Wazawa Crew na kujinyakulia shilingi laki 5.

Nkurlu aliyapongeza makundi yote hata ambayo hayakufanikiwa kushinda na kuyatakia kila la heri na yatipange upya kwa mwakani kwani asiye kubali kushindwa si mshindani aliongeza kuwa, kwa vile vijana hao wamejiweka katika mazingira ya kutumia vipaji vyao kujipatia ajira, Kampuni ya Vodacom-Tanzania inaona fahari kudhamini shindano hilo wakisaidia juhudi za serikali kupambana na tatizo la ajira.

“Takwimu zinaonesha kuwa kila mwaka vijana zaidi ya 800,000 wanaingia katika soko

la kusaka ajira ndio maana, Vodacom Tanzania kwa kulitambua hilo, tumekuwa mstari wa mbele kusaidiana na serikali na wadau wengine kuwajengea vijana msingi,” alisema Nkurlu.

 001.FINAL 002.FINAL 003.FINAL 004.FINAL 005.FINAL 006.FINAL 007.Fainali

Related Posts

Leave a Reply