Kwanini Mpenzi Wako Anakudanganya?

Uchunguzi unaoshangaza  juu ya udanganyifu kwenye mahusiano

Steven alikuwa ni msimamizi wa stoo kubwa , mahali ambapo  mizigo ilikuwa inawekwa. Alikuwa ni mtu anayependa juice ya  parachichi.

 Alisema kuwa amekuwa na tatizo la kutokosa kwenda kwenye  game, na hakutaka mke wake afahamu hilo,  aliogopa kuulizwa maswali mengi , na kwa uhakika hakutaka kumpoteza mke wake na kupata huzuni kubwa. Alielezea.

Mara nyingine nacheza  michezo  ya  bahati nasibu  online

Kwa ajili ya pesa?

Alisema ndio, lakini mara nyingi nashinda, na nafikiria kuacha mapema

Una kiasi gani ndani ya hilo shimo?

Kiasi cha  milioni hamsini na tano

Sema tena,

Lakini nitalipa kila kitu .Unafikiria ni vizuri kama nikimwambia mke wangu?

Kuepuka  mabishano au ni kulinda hisia

AngryWoman_1 KWA NINI MPENZI WAKO ANAKUDANGANYA

Steven alisema kuwa hataki kumchanganya mke wake  ni moja ya sababu iliomfanya adanganye. Alisema hakufikiria kama mke wake angeweza kumuelewa. Au angeweza kupata hasira  isio kuwa na sababu. Lakini hizi zote zilikuwa ni kujitetea.

Ni rahisi kwa mwanaume  kusema anamlinda mke wake  kwa  kumweka kwenye giza, lakini unafikiri angependa kufahamu kuhusu deni la nyumba yao? au unafikiria angependa kusikia kuwa ulipitiwa na kulala na mwanamke mwingine? Asilimia mia asingeweza . Lakini  sababu ambayo hakutaka kumwambia  ni kwa sababu hakutaka kuacha kucheza mchezo wa bahati nasibu. Na alikuwa hataki kugombana na mke wake , watu wengi hawapendi kugombana  ni rahisi kudanganya kuliko kusema ukweli.

Udanganyifu kwa ajili ya mapenzi

Binadamu pia wanadanganya  kwa sababu wanapenda. Nia ya kutafuta   mwenza  huwa ina mambo mengi, kujiweka tofauti, kuiga mambo yasio yako, kusema uongo. Udanganyifu ulio zidi  ni ule wa kudanganya  hali ulionayo kimaisha , kumbe sio hali yako ni ya mwingine, kujifanya una kila kitu  kumbe sio.  Mtu anaweza kuwa hana tabia hio lakini anajifunza kwa ajili ya kutaka kumpata mwenza. Hajali  na wala hakumbuki kuwa upo wakati itajulikana.  Na  hapo italeta matatizo makubwa. Wakati mwingine  hubadilisha ongea , mavazi ili kuwavutia wengine. Yapo mambo mazuri ya kuiga lakini sio ya kudanganya.

Kumbuka msingi wa mahusiano mazuri ni uaminifu. Kama utamvutia mwenza wako  ambae unahitaji kuishi nae baadae  hutapata unachokitaka. Ni uongo  na udanganyifu mkubwa . Maana itakuja julikana kwamba wewe sio wa vile. Ni wa aina hii.

Watu wanasema kuwa  wanaaminiana  na wenza wao  lakini hawakubali hali halisi, uongo wao ndio unaokubalika, hii inaacha mlango wazi kwa ajili ya tafsiri, inategemea na hali iliopo. Kwamba hawezi kujua hiki na kile,

Ni asilimia kubwa ya wanaume ambao wanasema kuwa ni bora kudanganya ili  kusiwe na ugomvi mwingi. Lakini sio uamuzi mzuri  , kinachotakiwa ni uaminifu .Sio kudanganya kwa ajili ya kutaka amani kati yenu. na ukweli ndio huo kuwa mwanaume siku zote ana siri  na anaweza kukuangalia machoni   na ukajua kuwa anasema ukweli.

Wanaume huwaogopa wanawake , kwa sababu wanawake  tunapenda kuongea sana, na hio inaweza kuwa ndio sababu ya kudanganywa.

Nafikiri ni vizuri kuwa mkweli kwa kila kitu  unachojisikia na kufikiria .  hii italeta uhalisia wako na kuonyesha uaminifu wako.

Credit : www.lizzdavid.com

Related Posts

Leave a Reply