So last weekend ilikuwa ndo ile event ya Fahamu Talk na 8020fashions tulikuwa wadhamini na of course ,Mie Middy ndo niliwakilisha blog kule kwenye Event .Ilifanyikia pale Nkrumah Hall UDSM .
Mc wa shughuli alikuwa the comedian Evance Bukuku
Event ilikuwa na vyote ambavyo nilitariajia na ambavyo sikutarajia,binafsi sijawahi kwenda kwenye events za Hivi vichwa viwili but am glad i went and learned a lot ,yani nawaza kwanini events zao zingine sikuwa na attend.
Mgeni Rasmi alikuwa Mh.Balozi mstaafu Balozi Patrick Tsere na Kamishna mstaafu wa kanda maalum Mh.Suleiman Hussein Kova
FAHAMU TALK
Ufahamu basi walisema ni uwezo wa kujitambuaa,kupokea mambo mapya,kuchanganua na kuongeza upeo wako.
1.FINANCIAL FREEDOOM FOR A BETTER LIFE -Anthony Luvanda
2.JINSI TOFAUTI ZA KIJINSIA ZINAVYO ATHIRI MAHUSIANO-Dr.Chris Mauki
Haya ndo nilojifunza Kwenye Mada ya Financial freedom for a better life
Kikubwa ni kuwa Pesa ni idea ,kuwa tu na idea ya biashara fulani au kitu flani ambacho kitakuingizia fedha basi hiyo ni pesa tosha.Una anza na idea kwanza .So pesa ina anzia kichwani kwako before kuipeleka kwenye utendaji.
Money will not make you rich your behaviour will ,hapa alifocus kwa wale ambao unakuta unapesa but una fulia haraka au maisha yanakuwa magumu kila siku na unakuta unaongezewa mshahara ni sababu huna discipline na fedha matumizi ambayo yanakuwa sio ya lazima au muhimu.
Kingine ni kwamba kuwa na too much money ni tatizo na kuwa na less money ni tatizo sana,na huwa wanasemaga Pata hela tujue tabia yako.
Akaongelea pia issue ya Assets na Liability
Asset ni kitu/vitu vinavykuletea au kukuingizia fedha
Liability ni kuwa na vitu ambavyo havikuingizii fedha mfukoni mwaka
So ukitaka kununua kitu jiulize hiyo ni Liability au Asset???sio unakopa mkopo wanda nunua iphone 7 au kuanzia maisha jamani msijaribu ,kopa ufanye kitu kitachokuingizia fedha .
Badilisha maisha yako acha kununua makorokoro yasiyo na muhimu tena kama wadada sisi una pochi 100 mbaya hazina quality wala nini ni heri hiyo hela basi ununue pochi hata 5 tu nzuri.
Develop multiple sources of income ,usisubiri tu mshahara au kutegemea chanzo kimoja cha fedha tafuta vingine.
Kingine uwe na marafiki wanao ku inspire maana kuna watu mnamarafiki ambao ni majanga hawawezi hata kukushauri kufanya vitu vya maendeleo.
Mwisho basi Take action on how you spend your money,make the right decisions ,stay committed and focused
Walokuwepo am sure mli enjoy alitoa mifano hai ,lugha ilieleweka na kwakweli am going there was worth it.
For the Dvd za Inspirational talks follow Tonyinspirationaltalk
JINSI TOFAUTI ZA KIJINSIA ZINAVYO ATHIRI MAHUSIANO-Dr.Chris Mauki
moja ya mada ambazo muda mrefu nilikuwa natamani kuzisikia zaidi.
So Dr.Mauki yeye alielezea kwamba jinsia zetu tu utofauti wake kwamba Mke au Mme ni sababu tosha ya kuathiria mahusiano,lazima ujue hizi toafuti kwanza la sivyo kila siku kutakuwa na majibizano,malumbano break ups hazitaisha.
Nilipenda alivyogusia kwamba kuna vitu kusema ukweli haviendi bila fedha hii haina ubishi mfano wataka mpeleka mpenzi wako holiday you need money au huko parefu hata nguo tu kumnunulia wahitaji hela .
Kuna mfano alitoa wa kwamba unatakiwa ukicheki menu ya chakula uangalie kutoka kulia kwenda kushoto na sio kushoto kwenda kulia akimaanisha una angalia chakula ndo price sio price then chakula.Kama huwa wa anglia price then chakula hali ni tete .
kwenye jinsia kuna TOFAUTI NA MATATIZO
Tofuati ni jinsia kuwa tuko tofauti Wanawake na wanaume
Matatizo ni kama vile Makuzi jinsi mtu alivyolelewa,Marafiki hawa wanabadilisha sana watu,background,Taalum etc
Ukikutana na Jinsia basi watakiwa kuwa muelewa ,na unachukiana nayo but Matatizo unayatatua
Chanzo cha Tofauti
1.Ubongo wanaume wako less connected kwamba hawawezai fanya mambo mengi kwa wakati mmoja
wakati wanawake wako very highly connected ndio wanaweza kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.
2.Kutostick na plan hapa wadada ndo tumejaa ,mara nyingi tunashindwa kustick to the plan waenda sokoni kununua mapazia but ukarudi na kapeti which is vice versa na wanaume ambao kama anaenda nunua viatu hata angalia hata mashati
Yapo mengi but leo naomba wasilisha haya tu
waweza pata CD za Audio na Dvd kuhusu hii mada kwa Dr.Chris Mauki follow him kwa instagram