Ligi ya Vyuo Vikuu kutimua vumbi jijini Mwanza

Ligi ya Vyuo vikuu vilivyopo mjini Mwanza itaanza kutimua vumbi jijini humo hivi karibuni ikiwa ni mkakati wa kuibua vipaji vya wanamichezo wasomi uliobuniwa na  Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustine (SAUT) kampasi ya Mwanza.
Kuanza kwa ligi hiyo kulitangazwa jana na Padre Leons Maziku, Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino Padri Leons Maziku, ambaye pia ni mratibu wa michezo katika Chuo hicho katika hafla ya kupokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
“Nashukuru Vodacom kwa kutuunga mkono katika kuendeleza michezo  na  napenda kuwatangazia wadau wote na wapenda soka kwa ujumla kuwa ligi hii ambayo ina lengo la kuendeleza michezo maandalizi yake yanaendelea na itafanyika katika Chuo hiki cha SAUT na itaanza katika siku za hivi karibuni”.Alisema.
Akikabidhi msaada wa vifaa hivyo, Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa Dominician Mkama, alisema kuwa Vodacom inayo furaha katika kushiriki kudhamini michezo hiyo ya wasomi kwa kuwa moja ya mkakati wake ni kuendeleza michezo na Sanaa nchini.
“Vodacom Tanzania tayari tunatambua kuwa sanaa na michezo inaweza kuinua  hali ya maisha ya vijana kwa kupunguza tatizo la ajira ndio maana tulipopata  ombi la  kudhamini mashindano haya tulilifanyia kazi kwa haraka na tunaendelea na mkakati wa kudhamini michezo nchini ikiwemo Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania na mashindano ya kudansi yanayojulikana kama”Dance 100%”.
Aliwataka vijana popote walipo nchini kuchangamkia fursa za michezo na utamaduni kwa kuwa ni eneo ambalo bado lina nafasi ya kutoa ajira na kuinua maisha yao kama ambavyo tumeshuhudia wachezaji wa michezo mbalimbali na wasanii wana maisha mazuri kutokana na kazi hizi.
“Baadhi ya sanaa na michezo kama vile kucheza dansi,kuimba nyimbo,kucheza mpira wa miguu,kucheza tenesi,kucheza mpira wa mikono,riadha,mpira wa pete,bila kusahau tasnia ya filamu ambayo wasanii wengi waTanzania wamekuwa na mwamko nayo hivi sasa ni ajira tosha kwa vijana ikifanywa kwa umakini na wadau kuwawezesha washiriki na serikali inaweza kupata mapato kupitia fani hizi”Alisema Mkama.
 Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,Dominician Mkama(kushoto) na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha jijini Mwanza,Padri Leons Maziku(kulia)pamoja na wanafunzi wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha jijini Mwanza wakiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)baadhi ya vifaa vya michezo,Vilivyotolewa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya mashindano ya  ligi ya Vyuo vikuu itakayoanza kutimua vumbi jijini humo hivi karibuni.
001 (1)
   Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,Dominician Mkama(kushoto) akimkabidhi tisheti  Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha jijini Mwanza,Padri Leons Maziku(kulia)na vifaa mbalimbali vya michezo,Vilivyotolewa msaada na Vodacom Tanzania kwa ajili ya mashindano ya  ligi ya Vyuo vikuu itakayotimua vumbi jijini humo hivi karibuni.
002 (1)
003 (1)
 Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza,Padri Leons Maziku(kulia)akimfafanulia jambo Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa,Dominician Mkama(kushoto)baada ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya michezo chuoni hapo kwa ajili ya mashindano ya  ligi ya Vyuo vikuu itakayotimua vumbi hivi karibuni jijini humo.
004 (1)

Related Posts

1 Comment

  1. Me and my friends are looking for Fr. Leons N. Maziku since 1997 after college graduation in the Philippines. Would it be possible to reach him? Can anyone provide my email to him? Thank you.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.