M-pesa kuwezesha uwekezaji UTT

hamana ya Uwekezaji Tanzania – UTT imetangaza kuanza kutumia huduma ya M-pesa katika kuwawezesha watanzania kununua vipande vya mifuko ya pamoja iliyo chini ya UTT ikiwa ni katika jitihada za kuwawezesha watanzania kuwa na njia rahisi na iliyo salama katika kufanikisha azima yao ya kujijengea maisha bora ya baadae kwa kujiwekea akiba.

Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim  amesema UTT inaungana na mamia ya watoa huduma nchini ambao wameona fursa iliyopo kwa M-pesa katika kurahisisha huduma na kupunguza gharama za uendeshaji na ufikiwaji wa huduma kwa upande wa wateja

Ukuaji wa M-pesa umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi ambao sasa wana nafasi kubwa ya kukamilisha shughuli zao nyingi za kijamii na kiuchumi kupitia simu zao za mkononi.

“M-pesa inaendelea kuwaleta watoa huduma na wateja karibu kwa namna ya kipekee huku tukidhihirisha jinsi ambavyo tunavyotumia teknolojia ya simu za mkononi kuboresha maisha ya watu. Hii ni azima yetu ya wakati wote na tutaendelea kuwa wabunifu.”Alisema Mwalim

Mwalim amesema M-pesa imeendelea kuwa kinara katika huduma za kifedha kwa njia ya simu ya mkononi na kuipongeza UTT kwa kuungana na familia pana ya M-pesa ubia ambao amesema utakuwa na manufaa makubwa kwa kila upande.

“M-pesa ina mawakala zaidi ya 70,000 nchi nzima, inawafikia watanzania wengi zaidi mijini na vijini kuliko huduma nyengine yoyote ya ina hiyo. Hali hii itawasaidia sana UTT kuboresha biashara huku ikiwawezesha watanzania wengi zaidi kuwekeza katika mifuko inayoendeshwa na UTT.

Kwa upande wake Afisa Mwendeshaji Mkuu wa UTT Bw. Simon Migangala amesema ubia na M-pesa utapanua wigo wa UTT katika kuwafikia watanzania na hivyo kwa kuwapatia njia mbadala ya malipo.

“Tunafuraha leo kuona tunaboresha njia za uwasilishaji wa akiba na uwekezaji wanaoufanya katika mfuko kwa kuwapatia njia mbadala. Ni dhamira ya mfuko kuona kwmaba inakuja na njia bora za kuwawezesaha watanzania wengi zaidi kunufaika na kile tunachokifanya kwa ajili yao.”Alisema Migangala 

Amesema miaka 11 baada ya kuanzishwa kwa UTT imenfanikiwa kuanzisha na kuendesha mifuko mitano ikiwemo Mfuko wa Umoja (2005), Mfuko wa Wekeza Maisha (2007), Mfuko wa Watoto na Kujikimu (2008) na Mfuko wa Ukwasi (2013).

Kwa ajili ya kutekeleza azma yake, Leo hii  UTT inashirikiana na kampuni ya Vodacom ili kuweza kupanua wigo wake ili kuweza kuwafikia na kuwanufaisha  watanzania wengi. Kuanzia sasa wawekezaji  wanaweza kuwekeza kwa kupitia mtandao wa Vodacom.

Dhamana ya Uwekezaji Tanzania ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2003. Dhumuni kuu la kuanzisha Taasisi hii ni kuwahamasisha Watanzania katika kuweka akiba na uwekezaji kwa kuanzisha Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Collective Investment Schemes).

Mifuko hii ina wawekezaji zaidi ya laki moja na kumi na thamani ya mifuko hii ni zaidi ya Shilingi bilioni 170.

001.UTT

Afisa Mkuu Mwendeshaji wa  Dhamana ya Uwekazaji Tanzania (UTT) Simon Migangala  akifafanua  jambo  kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na wateja wa mfuko huo watakavyonufaika na utumiaji wa  huduma ya M-Pesa itakavyowawezesha wananchi  kununua Vipande vya mifuko ya Pamoja iliyo chini ya UTT   kwa njia rahisi na salama katika kufanikisha azima yao kujijengea maisha bora ya baadaye kwa kujiwekea akiba.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa  Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalim.Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.

002.UTT

Meneja Uhusiano wa  Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalim (kushoto)akionyesha  kipeperushi kinachoelezea  jinsi wateja  wa  Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT)  watakavyotumia  huduma ya M-pesa kwa kununu vipande vya Mifuko ya Pamoja iliyochini ya UTT kwa njia rahisi na salama katika kufanikisha azima yao kujijengea maisha bora ya baadaye kwa kujiwekea akiba.Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

003.UTT

Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT)  Issa Wahichinenda(katikati)akishuhudiwa na Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim(kushoto)na Afisa Mkuu Mwendeshaji wa UTT Simon Migangala akielezea jinsi  wateja wa mfuko huo watakavyokuwa wakitumia huduma ya M-PESA  kwa kununu vipande vya Mifuko ya Pamoja iliyochini ya UTT kwa njia rahisi na salama katika kufanikisha azima yao ya kujijengea maisha bora ya baadaye kwa kujiwekea akiba. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Related Posts

Leave a Reply