MAHOJIANO NA WADADA WA KIKUNDI CHA MANYATTA HOUSE OF ACCESORIES

Interview ilikuwa hivi

1. Manyatta ni jina la kimasai lina maanisha nini?
Ni kweli Manyatta ni neno la Kimasai. Katika lugha ya Kimasai, Manyatta ni makazi/nyumba ambazo zinajengwa na wanawake wa kimasai katika uwanja au kambi kwa ajili ya kuishi mashujaa, kwajina linguine Morani.MM

2. Majina yenu wote na Kama mna members wengine na kazi zao/functions za kila mmoja wenu.
Manyatta imeundwa na wadada watatu ambao ni Antonia Kilama, Nancy Bondo na Sakina Mbullo. Pia imeajiri watu watatu ambao husaidia katika kazi za utengeneza bidhaa, uuzaji na usafirishaji.

Hii safi mbali na kujiajiri wameweza kuajiri vijana wenzao big up .MN

3. Mko wadada wa tatu nani alikuja na hii idea?
Idea ilikuja kwetu sote baada ya kutembelea duka moja kule Mwenge. Mwanzo tulikuwa tunajihusisha zaidi katika uuzaji wa bidhaa, yaani accessories, kutoka nje. Ila baada ya kutembelea hilo duka, tukajiuliza kwani na sisi tukijaribu kazi za mikono tutashindwa? Tangu siku hiyo, mpaka leo, tumeweza kuendeleza ubunifu wetu na fani yetu katika uwezo ambao hatukuutegemea kabisa.

IMG-20150918-WA0011

KAZI ZAO

IMG-20150918-WA0010

4. Mambo ya shanga mmesomea Art au ni ubunifu wenu tu.
Mambo ya shanga ni ubunifu na utundu wetu tu. Hatujasomea. Ila tuna mpango wa kwenda kupata hata lessons mbili tatu kuendeleza ujuzi.

Kuongeza ujuzi ni jambo la muhimu sana kwa mjasiriamali yoyote.IMG-20150918-WA0009

5. Inspirations zenu mnapata wapi?
Kwa kweli kila mmoja wetu ana utundu wake na utundu huo unatusaidia katika designs zetu. Kwa mfano tunaweza kuona rangi, hata mbegu za tunda na jinsi ziliyojikusanya, kwamfano mbegu za papai, na tunaanza kuwaza designs za accessories. Inspirations huwa zinatoka popote. Kila kitu ukikiangalia katika jicho la kutafuta inspiration, kina kuwa inspiring.IMG-20150918-WA0007

6. Nini kime wa inspire kwenye Shanga
Shanga kwa miaka mingi zimekuwa kama urembo wa Kiafrika. Mnakumbuka kitabu cha No Longer at Ease? Yule dada na shanga zake? Sasa tangu enzi hizo kitabu kilipoandikwa mpaka leo, shanga hazijapoteza fashion yake, na zitaendelea kuwa trendy mpaka mwisho. Shanga hazichakai, zipo colorful, zinapendezesha na ni pride ya Africa.

IMG-20150918-WA0004

7. Mawasiliano yenu Physical address, instagram name, emails, namba za simu.
Address: MANYATTA: House of Accessories,
Sinza, Palestina,
Dar es Salaam
Mtaa

Instagram Name: @manyatta_101
@beadsbymanyatta

Email: manyatta101@gmail.com

Mobile No. +255 754 655 146

8. Changamoto mnazo kutana nazo kwenye biashara
– Upatikanaji wa affordable quality material. Ili kutuwezesha kutengeneza affordable quality products. Tunahitaji bidhaa kama hizi.
– Kila mmoja wetu kaajiriwa, usiombe umepata order lukuki alafu mwajiri pia ana kazi nyingi kuliko kawaida,
– Sisi ni marafiki, ni ngumu saa nyingine to draw that line between friendship and business. Though hii ni changamoto, it’s also one of our strength.

IMG-20150918-WA0006

9. Upatikanaji wa material ukoje?
Upatikanaji wa materials ni mgumu sana. Kuna raw materials nyingi tunahitaji ambazo hazipatikan aidha Dar es Salaam au nchini kabisa. Ikifika stage hii, inabidi kusafiri. Kama shanga tunanunua aidha hapa Dar es Salaam, Arusha, Nairobi, South Africa..
Katika beading, kuna jewellery findings, vile vyakumalizia aidha mkufu, hereni, bangili, n.k., hivi huwa tunaagiza. Havipatikani hapa nchini.IMG-20150918-WA0002

Mkawaungishe wadada hawa na kuwapa support .

Related Posts

2 Comments

  1. manyata nmependa kaz zenu hongeren sana.nami napenda kujifunza kutengeneza shanga munaweza kunisaidia?

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.