How to Make a Sweater/Top/Skirt Less Itchy( Nguo ambayo ukiiva inafanya Ujikune/Inawasha/Kuchomachoma)

Kuna nguo tunanunua zinakuwa na material flani hivi yanayofanya ukiivaaa lazima inachoma choma na kukufanya ujikune mara kwa mara na usikae kwa raha.Maana nguo kama hii inachokupa ni adhabu,waweza chagua kuacha kuivaa ila kama uliipenda usiiache nakupa solution ya nini ufanye kupunguza muwasho au kuchoma choma  kwa nguo hiyo,hii sana sana inatokea kwenye masweta.

Mahitaji ni machache tu ambayo hata nyumbani kwako unayo.

1.Vinegar au Baking Soda

2.Conditioner/shampoo

3.ziplock bag

STEP ONE::  chukua sweater/top au skirt yako loweka kwenye maji changanya na Vinegar kama huna weka baking soda ,loweka kwa muda wa dakika 30 hivi.washing-towel-or-clothing-by-hand
vinegar-imagevinegar

STEP TWO::loweka tena sweater lako kwenye shampoo au conditioner loweka kwa lisaa limoja ,then fikicha vizuri ,kisha suuza na kung’uta anika.

delon_aloevera_conditioner

STEP THREE::Likishakauka chukua ziplock bag inayotoshea nguo yako funga weka kwenye freezer kwa usiku mzima,likitoka hapo litakuwa kama haliwashi tena ,Mkishafanya hii mje mtuelezee how did it go,tujifunze wote kwa pamoja kizuri kula na wenzio.

New-Design-30x40cm-Rose-Printed-Zip-Lock-Bags-Clothing-Plastic-Package-Bag-5pcs-lot-Self-Sealing

Related Posts

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.