MAKUNDI MATANO YAINGIA FAINALI YA DANCE 100%

SAFARI ya shindano la Dance 100% imefikia patamu ambapo hapo jana makundi matano kati ya makundi kumi yaliyochuana vikali katika nusu fainali ya shindano hilo kwenye uwanja wa Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam.Shindano hilo linaloandaliwa na kituo cha televisheni cha East Africa(EATV) na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania limeleta mapinduzi makubwa katika tasnia hii na kuweza kuwavutia vijana wengi kushiriki.

Makundi ya wachezaji wa miondoko mbalimbali ya muziki ambayo yamefanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho cha fainali ni Wazawa Crew,Best Boys Crew,The W.T,Wakali sisi na The winners Crew.

Mratibu wa mashindano hayo,Happy Shame,alisema kuwa katika kinyang’anyiro cha nusu fainali hiyo wamefanikiwa kupata makundi 5 yatakayoingia  moja kwa moja kwenye fainali itayofanyika hapo baadaye.

“Huu ni mwaka wa tatu EATV tunaandaa mashindano haya chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania mwaka huu mashindano haya yamekuwa na umaarufu mkubwa na ushindani wa hali ya juu na kuwavutia vijana wengi ambao hujitokeza kushiriki”Alisema Shame.

Shame, aliongeza kuwa kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya ambayo pia yamekuwa yakioneshwa na kituo cha EATV kila jumatano saa  moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi Milioni 5.

Naye Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa shindano hilo,Matina Nkurlu aliwapongeza vijana wote walioshiriki katika shindano hilo na kuwapa moyo wale ambao hawakufanikiwa kuingia fainali kuwa wasife moyo kwani asiyekubali kushindwa si mshindani bali wajipange upya na wawe wabunifu zaidi na kuweza kushiriki tena hapo mwakani.

Alisema kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kwani muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.

“Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa”Anasema Nkurlu.

Pia alitoa wito kwa wakazi wa jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika fainali ya shindano hilo itakayofanyika hivi karibuni kuweza  kuwatia moyo vijana watakaotoa burudani kali na pia kununua bidhaa mbalimbali za Vodacom zitakazopatikana kwa bei nafuu kabisa katika shindano hilo kama vile Modem na Simu aina ya Samsung E1205 zote zikiuzwa kwa shilingi 25,000 tu”Alisisitiza Nkurlu.

 

002.NUSU FAINALI 0003.NUSU FAINALI 004.NUSU FAINAL 005.NUSU FAINAL 006.NUSU FAINAL 007.NUSU FAINAL 008.NUSU FAINAL 009.nusu fainali

Related Posts

Leave a Reply