Mambo 10 Alojifunza Faraja Nyalandu mwaka 2017 ,Trust me hata wewe unayahitaji

Yes kwa mwaka 2017 kuna mengi kila mmoja wetu amejifunza na amepitia ,matumaini ni ku make sure kwamba umejifunza na umejijenga kutokana na hayo ulopitia.

Faraja Nyalandu ali share kwenye page yake ya instagram mambo 10 ambayo amejifunza kwa mwaka ulopita ,kwakweli hata mimi nlipoyasoma kuna mengine nili relate kabisa na mengine nimejivunia kuyajua sababu sometimes kuna mambo yanakutokea hujui maana au definitions zake but hapa Faraja anayadadavua vyema.


1/10. Thamani yako ni maradufu unapokuwa wewe. Katika dunia hii yenye ushawishi mkubwa wa kukufanya uishi kwa matakwa ya wengi, simama imara katika uhalisia wako. Baraka zako zinaweza kufika zikakutana na wewe uliyejiching chong zikahisi zimepotea njia na kurudi zilikotoka. Be you. Be real. Mungu hamtupi mja wake.

2/10 Unyenyekevu sio udhaifu. Watu wanyenyekevu ni watu wanaojiamini vya kutosha kuweza kumpa mtu mwingine nguvu na heshima. Anayejishusha, atanyanyuliwa. Be Humble.

3/10 Usiionee kazi yako aibu, own it, put your name on it. Usijisikie vibaya kujipongeza na hata kujisifu kwa kazi nzuri uliyofanya. Hakuna anayejua jinsi gani umepambana kufika hapo ulipo kuliko wewe mwenyewe. Jivunie na iambie dunia, unaweza ukawa ushuhuda kwa mwingine asiyejua inawezekana.
Kwenye picha ni @diarraeg akiwa amepokea tuzo ya @shuledirect ya best innovator of the year. Tuzo hii inatambua mtu anayefanya kazi Shule Direct, aliyetekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa. Aliyekuwa mbunifu na kujitolea kwa wengine zaidi ya kawaida. Mshindi anapatikana kwa kura za staff wenzake.

4/10 Sio kila changamoto utakayopitia ni ya kutatua, nyingine ni za kuzivuka kama zilivyo ili ujifunze. Kwa mfano kuna changamoto zinazoweza kutokea ili kukudhihirishia watu ulionao kwenye maisha yako. Kuna watu wamefika mwisho wa safari yao kwenye maisha yako au wewe umefika mwisho wa safari yako kwenye maisha yao na kuna matukio yatakufahamisha hivyo. Kubali yaishe, maumivu ya leo ni pona ya kesho. Move on to a better day!

5/10 Usiogope kufeli, ogopa kutokujaribu. Jifunze na makosa. Baba yangu alikuwa ananiambia mtu mwerevu hujifunza na makosa ya wengine, usisubiri mpaka yakukute.

6/10 ‘Choose people who choose you’ Watu wako wa karibu wana nguvu kubwa ya kukujenga au kukuangusha. Jitahidi uzungukwe na watu wanaokupa moyo, wanaokutakia mema na wanaofurahia mafanikio yako. Inakaa kama ni rahisi ila kwenye uhalisia ni ngumu. Sio kila aliye karibu nawe anafurahia hatua zako. Jitahidi wanaokufurahia wawe wengi kuliko wasiokufurahia. Mhenga aliyesema kikulacho ki nguoni mwako pengine angemalizia kikufaacho pia ki nguoni mwako. Choose your circle wisely.

7/10 Usikubali kila ‘Hapana’. Tafuta njia nyingine ya kumuonesha au kumhamasisha huyo mtu kukubali. Kuna watu watakwambia hapana kutokana na walichosikia juu yako. Kuna watakaokwambia hapana kwasababu kwa muonekano wako hufananii hiyo shughuli. Kuna wale wa hapana kwasababu tu pendekezo limeletwa na wewe, ila unachokipendekeza wanakitaka. Kajipange upya, rudi na mbinu tofauti. Kila hapana ina sababu, fanyia kazi hizo sababu.

8/10 Kuwa na moyo wa shukrani. Tushukuru kwa kila jambo, zuri au baya. Mungu hutumia changamoto kuonesha jinsi alivyo Mkuu. Na baraka zake hutimiza mazuri aliyotuahidi.

9/10 Mwaka 2017 niliamua nahitaji kujipa nafasi ya kuzisikiliza hisia zangu zote. Ili kufanikisha azma hii ikitokea jambo la kunihuzunisha, silazimishi kutokuhuzunika au kutokulia, nilikuwa radhi kulia ili nije nicheke. Nilikubali mimi ni binadamu mwenye hisia zote na hata nikichagua kuwa na furaha ni kwasababu nastahili kuwa na furaha. Kwasababu Neema ya Mungu ni kubwa kuliko huzuni. Nakumbuka kila nilipofiwa na mzazi wangu niliambiwa jikaze usilie, nilijikaza nikiwa na donge kifuani. Wasichojua miaka baada ya pale nimekaa nikalia. Sana. Peke yangu. Ishi kikamilifu. Ishi kila hali. Kuna wakati wa kufurahi na wakati wa kulia. Jitafute sana uweze kuchagua furaha. Hata ukilia ujue ni daraja la kuja kufurahi. Acha vyuma vikaze lakini sio sisi binadamu. We are humans. Break down. Rise up. Choose Happiness. Rise again.

10/10 Kila unalofanikiwa ni kwa neema ya Mungu. Wewe si bora kuliko aliyenyimwa. Sisi ni vyombo Vyake tu, kila mmoja na matumizi yake. Ukianza kuwa chombo kinachokufaa mwenyewe na si wengine au kusudi la Mungu, matumizi yanaweza kubadilika. Glory is all His. Glory belongs to God. I am so grateful for everything, every one, every experience that made 2017 yet another fulfilling year. All Glory belong to God.

Related Posts

1 Comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.