Mbinu 7 Za Kuchagua Mwenza Ambaye Hatakuacha.

Nimetambua kuwa  wakati wa kuchagua mwenza, watu wengi hupungukiwa na ufunguo  wa  kuamua kuwa siku moja nitapata mwenza ambaye hataniacha.

Kwanza watu wengi  hushindwa kuuliza maswali yanayohusiana na historia aliyokuwa nayo huyo mwenza kabla ya kukutana naye .Ni kosa kubwa sana. Jambo la pili Wanadharau tabia zinazojitokeza mwanzoni. Kwa kufikiria kuwa watamwogopesha mwenza ambaye anataka kuwa naye. Wengine husema kuwa hata kama kulikuwa na tatizo sihitaji kulifahamu. Lakini hapa kuna mbinu kadhaa za kukusaidia kumchagua mtu na kujitoa kwake.

1.Chagua mtu ambaye ana mahusiano mazuri -Alikotokea

Kutokana na historia yake ya huko nyuma itakuwa ndio dalili ya kuonyesha kuwa huyo mtu ana mahusiano mazuri. Kwa mfano huyo mtu kama anaishi vizuri na jamii yake, familia yake, wazazi wake, marafiki zake. Unaweza kujitoa kwake kwa sababu ni mtu mzuri, ana nguvu ya kutunza mahusiano.

2. Mchague mtu mwenye Mfano  mzuri  wa kuigwa.

Chagua mtu ambaye ana uelewa, hata kama ametoka kwenye familia ambayo wazazi wake waliachana, lakini  ni vizuri  kujua kama  ameathirika vipi kutokana na hali hio ya kutengana kwa wazazi wake. wengine hupata funzo kubwa  la kutatua matatizo yanapotokea kwa sababu ya  kuwa na uzoefu huo.  na atakuletea matokeo mazuri.lakini mwingine anaweza akawa ameathiriwa kabisa na matatizo hayo.

3.Chagua mtu anayeweza kuhandle Stress.

Mtu mwenye uwezo wa kukabiliana na shida mbalimbali huyo ni wa kushikana naye. Huu ni uelewa wa tofauti tena ni muhimu  kujitolea, kuwa mkweli na mtu mwenye kupenda umoja. Watu wenye hofu mara nyingi  huogopa kukutana na matatizo yanapotokea.  Ni rahisi kukimbia.

4.Mchague Mwenye Huruma

1 Mbinu 7 Za Kuchagua Mwenza Ambaye Hatakuacha

Mtu anayeweza kukuelewa maumivu yako na kukufanya ujisikie vizuri, ni mtu ambaye hataweza kukuacha unapokuwa unapitia aina yeyote ya tatizo.  Chukua mtu mwema na mwenye huruma , mtu mwenye moyo, na ambaye haogopi kufungua moyo wake kwako.

5.Chagua Mtu mwenye mawasiliano mazuri.

Niamini mimi. Ni vizuri kuwa na mtu anayeweza kuongea kuliko yule anayemeza maneno. Yule anayetambua umuhimu wa kuwasiliana kuliko yule anayetegea  mawasiliano. Siku moja dhoruba ikija  itawaangusha wote bila ya kujua ilikotokea.

6.Chagua mtu ambaye anapenda kuwa karibu yako , Kimwili na kihisia

Umbali ni mzuri ukiwa peke yako, na  huenda ni kitu ambacho unatakiwa kuepuka.  Chagua mtu anayependa kuwa karibu yako, anayependa kukugusa, mtu ambaye  anakukumbatia kwa mikono yake kwa muda wa kutosha, ambaye anapenda kukushika mikono yako, mtu ambaye anapenda kukubusu.  Kugusana inafanya kitu kizuri kwenye mahusiano.  Chagua mtu anayekufurahia uwepo wako, anayefurahia kuongea na wewe. Unapokuwa na mtu huyo hujisikii kuwa peke yako.

7.Chagua mtu ambaye mtakuwa na nia moja na thamani moja

11 Mbinu 7 Za Kuchagua Mwenza Ambaye Hatakuacha

Unaweza kumpata wa aina hii, lakini  mtu  ambaye  hana hamu ya kufurahia na wewe atakuboa. Anaweza akawa anatafuta mtu ambaye ana hamu naye. Kama wewe ni mchezaji wa mpira, tafuta mcheza mpira. Kama unaimba tafuta muimbaji,au anayependa unachokifanya.  Kama wewe ni Mchungaji tafuta mtu anayependa kuwa mama mchungaji.

Nakumbuka mama mmoja , wakati ambao aliolewa , mume wake hakuwa mchungaji, lakini kumbe ndani ya huyo mume kulikuwepo roho ya kichungaji. Ilipojitokeza, Mama huyo alikataa kuwa mama mchungaji. Alichofanya ni kuamua kuondoka. kwa hio tafuta mtu ambaye atapenda kitu unachokifanya.

Kufuata ushauri wangu sio kuwa na uhakika kabisa  wa kuepuka kuachwa,  Unaweza ukatafuta mbinu zingine nyingi za kutosha ili kuweza kutunza mahusiano yako. Uwe mwema kwa mwenza wako, Onyesha heshima kwake, Na uwe makini kila mara kucheki kama mambo yanaenda vizuri. Hapo ndio kukesha. Usilale ukitegemea kila kitu kitakuwa shwari.  tafuta mbinu, njia za kulea mahusiano. Nakutakia kila la heri.

Soma ushauri wamahusiano zaidi hapa chini

CREDIT : www.lizzdavid.com

Related Posts

Leave a Reply