Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu, superhero na zana (app) katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika

JUNI 16, 2017: Dar es Salaam, Tanzania. Katika maadhimisho ya Siku ya mtoto wa Afrika mwaka huu mtoto mwenye umri wa miaka sita Ethan Theodore Yona anayesoma darasa la kwanza amezindua zana yake ya android ambayo inaonesha shujaa wa hali ya juu akiwa ni muhusika anayejulikana kama EthanMan. Mhusika anaegemea upande wake na mwenye kipaji kikubwa, ameandika vitabu vya kuvutia, kubuni michezo ya kijifunza na kuwapeleka watoto katika safari za mafunzo.

Ethan alianza kujishughulisha na mradi huo alipokuwa na umri wa miaka mitano katika shule ya awali ikiwa ni matokeo ya mapenzi yake katika michezo na kujifunza. “Kila mara nilikuwa na nguvu nyingi ya kucheza, kufurahia kujifunza vitu vipya na kupenda kucheza michezo mbalimbali. Siku moja niliwaambia wazazi wangu ningependa kuanzisha mhusika mkuu jasiri kwa kuzingatia ubora wangu. Baadaye waliniuliza ubora huo ni upi na nikawaambia mimi nina kipaji kikubwa na ninaweza kuwa kitu chochote ninachokipenda, naweza kuwa mchezaji soka, nyota wa muziki, mhandisi n.k. Na hivyo ndivyo wazo la mhusika shujaa mkuu lilivyoanza.”

Ethan alifanya kazi hiyo na washauri wa teknolojia ya elimu kutoka i-Learn East Africa, ambayo inatoa kozi kwa njia ya mtandao na mafunzo ya mabadiliko, kuunda mhusika huyo anayejulikana Kama EthanMan, na kuanzisha kitabu chake cha kwanza cha picha alichokiita “Nitakapokuwa Mkubwa”. Tulivutiwa sana kufanya kazi na Ethan katika mradi huu. Inafurahisha kwamba mtoto mdogo namna hii kutaka kufanya jambo hili kubwa tulitaka kuwa sehemu ya huu mradi tangu mwanzo. Tukiwa ni kampuni ya ushauri katika masuala ya elimu tuliona umuhimu wa kujifunza ambao mradi huu utawapatia watoto. Mchango wa Ethan katika kuandaa kitabu hiki ni wa kushangaza,” alisema Ofisa Mtendaji wa i-Learn East Africa Bi. Noella Ntukamanzina.

Zana hiyo na michezo ilianzishwa kwa ushirikiano na kampuni ya Tujenge Tech ambayo imejikita katika kuanzisha masuluhisho ya kidijitali ambayo yatawezesha kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii.

“Tulipoombwa kuanzisha michezo ya EthanMan tulifurahi kuwa sehemu ya mradi huu wa kipekee kwani vitu kama hivi ndivyo vilitufanya kuingia katika teknolojia. Mchango wetu ulikuwa ni kuunganisha mhusika EthanMan na vipaji vyake vingi katika jukwaa ambalo litakuwa ni rahisi kufikiwa na kuwavutia watumiaji wakati. Mchango wa Ethan katika kuanzisha michezo ni wa hali ya juu, kwa sababu kila kitu kimejielekeza katika maisha yake kama mhusika. Tulikuwa na muda mzuri wa kuunda kile ambacho tunaamini kuwa ni bidhaa ya kwanza ya mchezo katika anga ya teknolojia nchini Tanzania.
Zana (App) ya EthanMan inapatikana kwa kupakua katika hifadhi ya michezo ya android (play store. Watoto wataweza kusoma vitabu, kucheza michezo na kufuatilia kwa karibu nyendo za muundaji wa EthanMan, Ethan Theodore Yona.

——- MWISHO——–//

 

Related Posts

Leave a Reply