Naibu Waziri wa fedha aitaka UTT MFI kufika vijijini

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameitaka Taasisi ya Utoaji mikopo na huduma za kifedha ya ‘UTT Microfinance’ kuandaa mpango mkakati wa kuwafikia wakulima vijijini na kuwapa mikopo itakayowasaidia kuzalisha mazao kwa wingi.
Akizungumza jana kwenye hafla fupi ya kuzindua rasmi bodi ya wakurugenzi ya Taasisi hiyo, Kijaji, alisema Tanzania ya viwanda inayotajwa pia itawategemea wakulima kufikia malengo hayo.
“naipongeza sana UTT kwa utendaji wake wa kazi na hasa kwa bodi hii iliyomaliza muda wake, kwa bodi mpya ninayoizindua leo iangalie namna ya kuwfikiwa wakulima vijijini na kuwapa mikopo nafuu ili kuborosha uzalishaji wake,” alisema Kijaji.
Aidha, alisema viwanda vitakavyoanzishwa nchini vingi vitategemea malighafi kutoka ndani ya nchi yakiwemo mazao ya wananchi vijijini.
“Serikali inataka kuona taasisi zake zoye za kifedha zilizoanzishwa zinatoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wananchi, hii itasaidia kuboresha maisha kwa mwananchi mmoja mmoja,” aliongezea kusema.
Alisema pamoja na mafanikio waliyoyapata UTT Microfinance kwa kipindi cha miaka mitatu, taasisi hiyo ijipange kutoa elimu kwa wajasiriamali na kuwaibua.
Awali akimkaribisha Naibu waziri huyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, James Washima, alisema Serikali haikufanya makosa kuanzisha taasisi hiyo kwa kuwa katika kipindi cha miaka miatatu tangu kuanzishwa kwake imewafikia zaidi ya wajasiriamali 23,513 huku kiasi cha shilingi bilioni 29.13 kilitolewa kama mikopo kwa wananchi hao. Alisema katika kipindi hicho matawi 12 yalifunguliwa katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Zanzibar na Dar es Salaam.
Bodi iliyozinduliwa na Naibu waziri Kijaji, inaongozwa yenye wajumbe wa nne inaongozwa na Mwenyekiti wa bodi Godwin Mjema, ambayo itakaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji (katikati)ambaye alikuwa mgeni rasmi akifafanua jambo katika  hafla ya Uzinduzi wa Bodi  Mpya ya  wakurugenzi wa  Taasisi ya Huduma za Fedha na Mikopo –UTT Microfinance PLC (UTT MFI) iliyofanyika makao makuu ya taasisi hiyo  leo  jijijni Dar es Salaam,Kushoto ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Godwin Mjema na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo,James Washima.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji (wapili kutoka kulia) akifafanua jambo wakati  wa   hafla ya uzinduzi wa Bodi  Mpya ya  wakurugenzi wa  Taasisi ya Huduma za Fedha na Mikopo –UTT Microfinance PLC (UTT MFI) iliyofanyika makao makuu ya taasisi hiyo  leo Upanga  jijijni Dar es Salaam. Kushoto ni ni mwakilishi wa Ofisi ya msaji wa Hazina Patrick Yegela , Mwenyekiti wa bodi hiyo Profesa Godwin Mjema na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo James Washima.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji (wapili kutoka kulia) akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Huduma za Fedha na Mikopo –UTT Microfinance PLC (UTT MFI) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi  Mpya ya  wakurugenzi wa  Taasisi ya Huduma za Fedha na Mikopo –UTT Microfinance PLC (UTT MFI)   Profesa Godwin Mjema   wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Mpya ya Wakurugenzi  wa taasisi hiyo iliyofanyika leo  makao makuu ya ofisi hiyo Upanga jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Huduma za Fedha na Mikopo –UTT Microginance PLC (UTT MFI) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashuta Kijaji wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Wakurugenzi iliyofanyika leo Upanga jijini Dar es Salaam.

Related Posts

Leave a Reply