Ndoto Hub Yahitimisha Mafunzo kwa Wanawake Wajasiriamali

NDOTO HUB YAHITIMISHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA
WANAWAKE NCHINI KUWAWEZESHA KIUCHUMI
Programu maalum inayoendeshwa na Ndoto Hub nchini yenye lengo la kuwawezesha
vijana wakike kiuchumi kwa kuwapatia nyenzo za biashara za kibunifu, nafasi na
maarifa ya kitaalamu yakufanyia kazi ndoto zao; imehitimisha mahafali yake ya
kwanza yaliyojikita kuendeleza Kilimo-Biashara na usindikaji wa vyakula ikiwa ni
hatua ya kuunga mkono kwa vitendo Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya
mwaka 2004.
Ndoto Hub imefanya mahafali hayo Jumatatu wiki hii kwa kufanya ziara katika ofisi
za Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ili kuweza kujifunza na
kutambua fursa zilizowekwa na serikali kwa ajili ya wajasiriamali nchini.
Akizungumza baada ya Mahafali, Meneja wa programu ya Ndoto Hub, Bi. Tulinagwe
Mwampanga amesema, ‘wamehamasika kuanzisha Programu hii kutokana nakuwepo
kwa changamoto zinazowakabili wanawake wajasiriamali katika kukuza biashara zao
ndani na nje ya nchi.’ Ndoto Hub inaamini katika kumuwezesha mwanamke ili kuleta
maendeleo katika jamii yake na kwa chachu ya maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Aidha, katika ziara hiyo, Ndugu Edwin Chrisant, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
amewapongeza wahitimu wa mafunzo hayo na kuwahamasisha kupeleka mipango
maalamu ya biashara zao ili kuweza kupata fursa ya kuwezeshwa mitaji na wadau
mbalimbali.
Mahafali haya, yalihitimishwa na tafrija fupi iliyofanyika jioni katika eneo la ofisi ya
Ndoto Hub huku ikihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo, wanawake na
ujasariamli. Katika tafrija hii, wahitimu waliweza kupata nafasi ya kuzielezea
biashara zao kwa wageni wa waalikwa na mhitimu Aisha Uzigo, aliibuka kuwa

mshindi katika maafali hiyo kwa kujishindia shilling millioni moja za kitanzania
zitakazomuwezesha kuanzisha biashara yake.

Zenna Kashaga, mmoja wa wahitimu aliwashukuru waandaji wa programu ya Ndoto
Hub na kuelezea namna ilivyomwezesha kujifunza ujasirimali na kuweza kumpa
mwongozo mzuri wa kujenga biashara yake, vilevile kumpa ujasiri, kujielewa zaidi na
kupambanua uwezo wake yeye kama mwanamke.
Kwa sasa Ndoto Hub inawakaribisha wanawake wote wenye mawazo ya kijasiriamali
katika mchepuo wa kilimo-biashara na usindikaji wa vyakula kutuma maombi ya
kujiunga kupitia www.ndotohub.com.

Related Posts

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.