Robo fainali ya Dance 100% yanukia

ROBO fainali ya mashindano ya Dance 100% 2014 inatarajiwa kufanyika Agosti 23 ikishirikisha makundi 16 kutoka wilaya tatu za Kinondoni, Temeke na Ilala, jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa jana na mratibu wa mashindano hayo, Happy Shame alipokuwa akizungumza na mwandishi wa gazeti hili na kufafanua kuwa katika robo fainali hiyo watapata makundi kumi bora yatakayoingia kwenye nusu fainali hapo baadaye.

Aliyataja makundi ambayo yamefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali kuwa ni  Wazawa crew,Best boys crew,G.O.P,The-W-T,Best love,Tatanisha Dancers,Bustani,Qulity boys,Pambana Fasaha,wakali sisi,Tamtam,Mazabe,TWC,B2K na winners crew.

“Huu ni mwaka wa tatu East Africa Radio na East Africa Television wanaandaa mashindano haya kwa udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania na kinywaji cha Grand Malta na yamekuwa yakipata vijana wengi ambao hujitokeza kushiriki,” alisema Shame.

Mratibu huyo alisema kuwa mashindano ya mwaka huu yalianza Julai 19 na kila yanapofanyika kwenye wilaya husika, yamekuwa yakirushwa East Africa Television kila Jumatano saa moja kamili usiku.

Alisema kuwa kundi ambalo litaibuka na ushindi litajinyakulia kitita cha Sh. milioni 5 na kwamba kila kundi limekuwa likijitahidi ili kuhakikisha kwamba litwaa kitita hicho.

Aidha, mratibu huyo alisema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakikosea kuandika jina la shindano hilo na kuwataka wawe wanmauliza ili kupata uhakika wa jina la shindano hilo kuwa ni Dance 100% 2014.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wa shindano hilo, Matina Nkurlu alisema kuwa wao wana jukumu la kuendeza shindano hilo kwa kutambua kwamba muziki ni ajira.

Alisema kuwa Vodacom Tanzania inajua ni jinsi gani serikali ilivyokuwa na majukumu mengi moja wapo likiwepo la kuwapatia vijana ajira kwa kutambua kuwa suala la ajira siyo lazima kuajiriwa kwenye kampuni ama viwanda au ofisini.

“Kwa kutambua hilo ndiyo maana sisi Vodacom Tanzania tumedhamini mashindano hayo kwani tunaamini kwamba baada ya hapo vijana hao wanaweza kuchukuliwa kwenda kutoa burudani sehemu mbalimbali na wakalipwa,”

alisema Nkurlu.

Meneja huyo aliwatia moyo vijana wanaoshiriki shindano hilo kwamba wasikate tamaa bali watambue wanachokifanya kinaweza kuwapa ajira hapo baadaye na kujikuta wakiendesha maisha yao bila wasiwasi.

02 06 (1)

Related Posts

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.