Shetta Mzee wa”Shikolobo” kubonga na wateja wa Vodacom”LIVE”

 Ni kupitia huduma mpya ya”Bonga na Staa”

Mashabiki wa mwanamuziki wa kizazi kipya wa bongo fleva Nurdin Billal alimaarufu kama Shetta watapata fursa ya kubonga naye Live Kutokana na kuzinduliwa kwa huduma mpya ya “Bonga na Star”iliyozinduliwa leo na Vodacom Tanzania mahususi kwa wateja wake.

Huduma hii ni kwa ajili ya wateja wote wanaotumia mtandao wa Vodacom inawawezesha  kuunganishwa na mastaa maarufu wanaowashabikia na kuweza kuongea nao moja kwa moja kupitia simu zao za mkononi katika siku maalumu zitakazokuwa zinapangwa na wateja kupatiwa taarifa kupitia simu zao za mkononi.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii ya aina yake Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema kuwa kwa mara nyingine tena Vodacom imekuja na huduma ya kuleta furaha kwa wateja wake itakayowapatia fursa ya kuongea live na mastaa wanaowashabikia .

“Kwa mara nyingine tena Vodacom tumewaletea promosheni hii ya aina yake ya kuwaletea furaha wateja wetu ukiwa na mwendelezo wa huduma mbalimbali za hapo awali ingawa hii ni tofauti kidogo kwa kuwa inawawezesha wateja wetu kuongea na mastaa wanaowashabikia Live ambapo wanaunganishwa nao na kuongea nao kwa gharama nafuu.Hii itafanyika katika siku maalumu zitakazopangwa ambapo wateja watakuwa wanafahamishwa mtu maarufu atakayekuwa amepangwa kabla ya siku kupitia simu zao na kwenye vyombo vya habari”Alisema Nkurlu.

Nkurlu aliongeza kusema “ Mastaa maarufu wenye washabiki wapo wa makundi mbalimbali wanaweza kuwa wachezaji wa mpira na michezo mingine,wanamuziki,wacheza sinema,wasanii wa maigizo na wengineo kinachotakiwa ili kuelewa jinsi ya kushiriki katika promosheni hii anachotakiwa kufanya mteja ni kununua tiketi ya kushiriki kupitia simu namba  0901766666 na kuunganishwa na huduma hii kupitia simu hiyohiyo na kuongea na  msaniii anayemshabikia kwa dakika moja.

Alisema kwa  anayehitaji kupata huduma hii anatozwa kiasi cha shilingi 150 ya kununua tiketi ili aunganishwe na shilingi 20 kwa kila dakika ya maongezi ambazo zinakatwa kutoka muda wa maongezi wa mtumiaji wa huduma.

001.chat 002.chat

Related Posts

Leave a Reply