I Stayed In A Bad Relationship For 3 Years/Nilikaa Kwenye Mahusiano Mabaya Kwa Miaka 3

“Nilikua katika mahusiano mabaya kwa miaka 3. Nilikua nashare mwanaume niliyekua naye na mtu mwingine. Alikuwa hapokei simu nikimpighia usiku, au ansema anafanyakazi hadi usiku sana. Ilikua ni miaka 3 ya kumfanya yeye ajisikie vizuri na kujiweka chini mimi. Nikawa najiambia kila siku kuwa labda nikijaribu zaidi naweza kuwa girlfriend mzuri, labda naweza kutengeneza mahusiano yetu yakawa mazuri na yenye furaha, labda nahitaji muda zaidi..lakini muda zaidi ulivyokuwa ukienda ndio nilivyozidi kukonda, niliisha sana, nilipungua pound 108 kutokana na stress. Nilikuwa muda wote nimeshika simu nikisubiri, nikiwa na hasira. Siku huyo mwanamke mwingine alichukua simu ya mwanaume niliyekua naye katika mahusiano na kunipigia, akaanza kuuliza maswali mengi, na ndipo nilipoamua siwezi kuishi hivi, nikaamua kuondoka. Ni mwaka 1 sasa umepita, sasa nina furaha, nimenenepa tena pound 20, Katika ile miaka 3 niliyokua nae yule mwanaume ilichukua kichekesho haswaa ndio uweze kunifanya nicheke lakini sasa naweza kucheka kitu chochote.”

depressed-black-woman

Hii story fupi kutoka humans of New York, huyu mdada ameelezea alivyokua ndani ya mahusiano na mwanaume asiyemjali, ameelezea kwa ufupi tu madhara aliyopata kutoka katika mahusiano hayo.

Tumeona ni kwa kiasi gani mahusiano yanavyoweza kukudhoofisha na kufanya usiwe na furaha katika maisha yako. Wapo wengi sana ambao wanakaa na wenza ambao hawawajali, hawawapendi, wanacheat lakini wenyewe wapo tu. Wanazidi kujilaumu wenyewe, wakijishawishi kuwa wao ndio tatizo, wakijaribu kutafuta kitu ili kumfanya yule mtu ambaye wapo nae katika mahusiano ajali. Lakini muda unavyozidi kwenda na wewe unayefanyiwa hayo mabaya ndio unaumia, unakonda, unajilaumu, unaishi na hasira na bila furaha.

woman

Point ni, mahusiano yanatakiwa kukufanya uwe na furaha lakini wanawake wengi wanashikwa kwenye mahusiano ambayo yanawafanya wawe wabaya au bila furaha.

Mara nyingine unakuwa hufahamu huyo mtu uliyekuwa nae amekufanya/amekubadilisha uwe mtu wa namna gani. Unakuwa unampenda sana huyo mtu kiasi cha kwamba unakuwa kipofu juu ya mambo mabaya anayokufanyia au unaamua kupotezea tu.

Couple-talking1

 Mahusiano yanatakiwa yakunyanyue, sio yakushushe. Mtu uliyekuwa nae anatakiwa akusaidie uwe the best version of yourself. Ni kweli kuwa katika mahusiano huwa sio furaha kila siku, mara nyingine mnagombana/kukorofishana lakini as long as mnajua jinsi ya kusuluhisha/kupatana/kuongea. Unatakiwa kuwa mvumilivu lakini sio katika kitu ambacho kinakuua polepole. Kila mwanamke anatakiwa kuwa na limit, haijalishi unampenda vipi huyo mtu wako, kama anafanya maisha yako kukosa furaha na unajiona kama wewe tu ndio mwenye makosa kila mara basi huyo sio wa kuwa nae.

Related Posts

2 Comments

  1. Kama umenisema mimi vile. Kuanzia February 12th, 2015 nimeamua
    ‘ku-move on’. Kuanzia hapo saa nyingine nasahau kuwa kuna wakati nilikuwa ninajiconsider kuwa nina mtu. Mtu asiyejali hisia zako. Mtu ambaye wote mpo Dar, lakini kama kuna long week end kuanzia Ijuma, Jumamosi, Jumapili, Jumatatu na kurudi kazini Jumanne, amini nakuambia, hakuna hata siku moja kati ya hizo atakutafuta japo kwa simu. Na wala usifikirie kwamba anajua amekukwaza na kwamba atarudi na kusema ‘hey babes, najua umekuwa mpweke, I am sorry, nilikuwa busy au nilipatwa na kile’; Nope. He wouldn’t do that na kwanza wala hafikirii kuna sababu ya kufanya hivyo. Jamani, niliwaza sana usiku ule wa tarehe 11 February, 2016. Nikasema moyoni, I need to take a decision. and I did and here I am today. Sina mtu, sitafuti, na wala sitegemei kutafuta kwa sababu sitaki kuumizwa tena. Lakini, nina furaha kwa sababu sina committment.

    Asante sana kwa kushare.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.