Ukweli kuhusu kifo cha Justice Jackson aliyeuwawa Huko Chuo Cha Saut baada ya Kutuhumiwa na kuitiwa Mwizi

12628099_1567878456836593_1410358701_n

So huyu kaka alitrend sana over the weekend na story ilikuwa kuna mwanafunzi ambaye ilidaiwa kuwa ni mpenzi wake but akamuitia mwizi akapigwa mpaka kufa na wanaosemekana kuwa ni wanafuzi wa chuo cha SAUT .

Kukawa na maoni kila mtu ya kwake wengi wakimshutumu huyo dada na mambo kibao but leo EFM wakawa wame air mahojiano ya Mama mzazi wa Jackson na Dada yake pamoja na HR /Msemaji mkuu wa chuo cha SAUT nilisikiliza na ntaelezea hapa kadri ntakavyoweza na kukumbuka mengi yalosema mpate tu picha kamili ya hii story.Na kama kuna mtu alisikiliza atanirekebisha ntakapokuwa nmesahau au kukosea maana mwisho wa siku huwezi kukumbuka kila kitu.

So mama wa marehem anasema alipigiwa simu jioni majira ya saa mbili kuwa mwanae anapigwa huko Saut kaiba sijui na awahi akichelewa atakuta kauwawa , wakaenda na dada wa marehem mpaka huko shule wakafika saa tatu wakakuta karibu gari ya polisi inaondoka but kuna mtu akasema mama yake huyu hapa wakaomba wamuone wakanyimwa but wakachungulia kwenye gari wakakuta kawekwa kichwa chini miguu juu kwenye gari  la polisi, wakaulizia mzima wakaambiwa mzima mtamuonea polisi
Wakaenda hadi kituoni wakizuiwa kumuona waka ambiwa waje kesho yake wakaondoka.12748226_461174850749772_919763557_n

 Asubuhi wakaenda kupeleka chai  hawakuongea nae wakaaulizia kama anaongea wakasema anaongea ,wasijali watampeleka hospital
So wakasema wasubiri pale pale polisi mpaka waruhusiwe kumuona but hawakuweza kwa siku hiyo.
Baadae kama sijasahau wakaambiwa waenda hospitali room no 5 ndo alikolazwa mnisamehe nmesahau jina la hospitali
Wakaenda hospital wamemtafuta sana room no 6 mpaka 8 sijui but wakamkosa
Wakarudi polisi wakasema walimuacha hapo waka angalie tena wakaenda wakamkosa basi wakajipa moyo kuwa kwakuwa hawamuoni na polisi walimuacha bila uangalizi atakuwa tu kwenye ward mojawapo wakaendelea kumtafuta wakamkosa
Kuna mtu akatoa wazo wakamuangalie mochwari basi yule mama akapigiwa tu simu sikumbuki nani alipiga simu wakamwambia mwanae alifariki asubuhi saa kumi na mbili Basi waka comfirm ikawa ni yeye kweli.

IMG-20160227-WA0008

Huyu dada ndo watu walizusha alikuwa mpenzi wake huyu kaka ila Msemaji wa chuo alisema huyo dada alimaliza hapo sauti Miaka Miwili au mitatu kama sijasahau hapo hapo Saut kwa hiyo sio mwanafunzi wa hapo.

Na huyu dada alikanusha kuwa hakuwa mpenzi wa huyu kaka.Huyu kaka alikuwa maarufu na am sure alipiga picha na watu wengi .
Upande wa chuo sasa wakaulizwa

Msemaji wa chuo  akasema kweli wanataarifa za huyo kaka na  huyo kaka alikuwa kibaka na aliiba simu mbili, Alipoiba hizo simu akatoka na hizo simu huyo msichana alokuwa anamhoji sijui nae ni kati ya waloibiwa au alikuwa akipita, akamuona yule kaka kasimama muda mrefu pale anamuuliza anafanya nini pale na kumuuliza kama yeye jackson ni mwanafunzi aksema sio mwanafunzi ila kuna dada anawasiliana nae hapo  kwa simu but yule dada akaendelea mhoji akasema au utakuwa nawe ni wale wezi akamwambia ampe namba za huyo anaemtafuta apige akasema piga tu yeye sio mwizi
Basi hapo sasa sielewi hawakumpata huyo mtu yule dada akaanza ita mwizi na yule kaka nae akaanza kukimbia ,kufika nje akauta wakaka kibao mmoja akamtega akaanguka buta akafanikiwa kuamka akaendelea kimbia but walimkamata na kumpiga sana
Huyo msemaji anasema alikabidhiwa kwa polisi wa zamu wa chuo na alikutwa kweli na simu hizo mbili maana dada ake alihoji hao waloibiwa ni kina nani na aliiba nini waambiwe  ,So akahojiwa akakubali aliiba na akaomba asamehewe na wale waloibiwa wakakiri ni simu zao hizo ,Polisi nako alikubali kweli aliiba na akaomba msamaha vile vile.
Utata sasa unakuja hapa msemji wa chuo anasema mpaka saa 6 usiku huyo kaka alikuwa chuo anahojiwa sijui na Mama WA marehem anasema alipigiwa simu saa mbili kuhusu mwanae kukutwa huko saut na kupigwa sasa hapa which is which ??bado kuna mystery
Mpaka wanatoa hayo maelezo  hamna mwanafunzi alokamatwa wala nini msemaji wa chuo anasema wamewaonya tu wanachuo wasichukue sheria mkononi na ilikuwa usiku walopiga hawajulikani.

This is very sad kwanini watu wajichukulie sheria mkononi ,huyu kaka sijui kama hata alipata wasaa wa kujieleza.

Mdau waonaje hii issue nini maoni yako??share nasi kwa comment below.

Related Posts

1 Comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.