UZINDUZI WA MNARA WA AIRTELL MUHUKULU SONGEA VIJIJNI

Mkuu wa Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Joseph Joseph  Mkirikiti
amezindua mitambo ya mawasiliano (minara) katikaka kijiji cha Muhukulu
na kuwataka raia wa Tanzania wa vijiji vya Muhukulu, Lalia, Magwamila,
Nakwale, Nambendo, Mkenda, Makwaya, Miputa  vyote vya Mkoani Ruvuma na
wale wote wanaoishi mipakakani mwa Msumbiji na Tanzania kuwa Walinzi
kwa mitambo ya Airtel inayowekwa kwa ajili ya mawasiliano isiharibiwe
na watu wasiopenda maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti ameyasema hayo
mwishoni mwa wiki wakati akizindua Minara hiyo ya ya mawasiliano ya
Simu iliojengwa katika kata ya Mhukuru Mpakani mwa Msumbiji na
Tanzania.

Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti alisema “juhudi
zinazofanywa na Serekari kwa kushirikiana na Makapuni ya Simu ikwemo
kampuni ya Airtel ni kumpa mwananchi fulsa ya  kuwasiliana na
watukatika mambo ya  kiuchumi,afya,na elimu  na mawasiliano ya kijami”

Amesema pia katika kutatua kero mbali mbali za wananchi, pamoja na
mawasiliano ndiyo maana baada ya ziara ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano
wa Tanzania wananchi walipotoa kero zao kwa Rais ufumbuzi umefanywa
wakuiomba Airtel kujenga Mnara ..
…”sasa ni juu ya Wananchi kuutumia kwa lengo lililo wekwa ili
kutowakatisha tamaa wawekezaji aliongeza kwa kusema Mkirikiti!
Meneja wa kanda ya kusini wa Airtel kutoka mbeya Straton Afrikan Mushi
amewataka wananchi kutumia mtandao wa Airtel hasa huduma za kibenki
ili kuepukana na uporaji wa fedha wanaposafili,  pia amewaomba kuwa
walinzi wa Minara ya Airtel ‘naomba mfahamu huu mtambo hapa ni
kwaajili yenu wote hivyo changamkieni huduma zetu nafuu Zaidi hasa ile
ya Airtel Money ambayo itaondoa na kupunguza changamoto nyingi za
upatikanaji wa huduma za kibenk katika vijiji na miji ya karibu na
mkoa wetu huu” aliongeza Straton

Wananchi wa Mkoani Ruvuma wameishukuru serikali kwa kuweza
kushirikiana na Kampuni ya Airtel kupata mawasilino ya uhakika huku
injinia wa Airtel  Saidi Hanga akiwaahidi  wananchi kuto katika kwa
mawasiliano

Mnara wa Simu wa Kampuni ya Airtel umekuwa mkombozi pekee kwa wananchi
wa Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania ambao walikuwa wakisafiri kwa
muda mrefu zaidi ya kilometa 40 kutafuta sehemu yenye kushika
mawasiliano kwa kupanda kwenye kilele cha mlima, pia wamesema
mawasiliano ya nchi jirani ya msumbiji ukiyapata yalikuwa yatoza fedha
pande zote mbili bila kujali nani kapiga simu nani amepokea simu.

DSC_0803 DSC_0804

Mkuu wa wilaya songea Joseph Mkirikiti akikata utepe
kuasiria ufunguzi wa mnara wa Airtel uliopo Wilaya ya Songea Mkoani
Ruvuma mipakakani mwa Msumbiji na Tanzania ili kuboresha mawasiliano
katika mkoa Ruvuma na jirani, anaeshudia ni meneja wa kanda ya Kusini
wa Airtel Bw Straton Mushi (wakwanza kulia) na meneja masoko wa kanda
hiyo wa Airtel Bw Jonas Mbaga (kati) mwishoni mwa wiki, mawasiliano
hayo yatazaidia vijiji vya Muhukulu, Lalia, Magwamila, Nakwale,
Nambendo, Mkenda, Makwaya, Miputa  vyote vya Mkoani Ruvuma

DSC_0820wananchi wakisangili mara baada ya Mkuu wa wilaya ya
Songea Joseph Mkirikiti kukata utepe kuashiria ufunguzi wa mnara wa
Airtel Mkoani Ruvuma mpakani mwa Tanzania na msumbiji kwa lengo la
kuboresha mawasiliano mwishoni mwa wiki,wawasiliano haya yatasaidia
vijiji vya Muhukulu, Lalia, Magwamila, Nakwale, Nambendo, Mkenda,
Makwaya, Miputa  vyote vya Mkoani Ruvuma

Related Posts

Leave a Reply