Video ya Zigo Remix ya A.Y ft Diamond Platnumz Yafungiwa na TCRA.

12479201_958522440908663_2125336933_nSo Video ya Zigo Remix imefungiwa  na TCRA baada ya kuitathmini Video hiyo nakuona haina maadili na taswira nzuri kwa jamii.
Akihojiwa, AY anasema amesikitishwa na hatua hiyo, sababu haoni kosa katika wimbo huo. AY anasema sehemu ya video ya wimbo huo ilichukuliwa katika “swimming Pool” hivyo ilikuwa ni lazima kwa watu kuvaa mavazi ya aina ile, lakini zaidi anashangaa TCRA kuufungia wimbo wake wa “Zigo” na kuziacha nyimbo nyingine za kutoka nje kama za kina Nicki Minaj ambazo zinaonyesha picha zisizo na maadili.

12552366_1526240334372469_943655540_n

vidoe ndo hii kama hukuona na Kwenye Tv ndo haionyeshwi tena 

Idriss Sultan katoa maoni yake kwa instagram page yake akisema ::

TCRA tufanye hiviiii, si tunawaachia kina Rose Mhando na kina Bahati Bukuku waimbe kwakweli na Msondo Ngoma. Kizazi kipya waende Kenya na Sauzi na Nigeria. Vitu vingine vidogo sana tunakaziana. Tuoneeni huruma sometimes maana kwa hali hii hizo tuzo za nje si watabaki nazo maforena huko. Kuzuia mabadiliko ya kimziki sio kuhifadhi utamaduni wa Mtanzania. Kufundisha utamaduni wa mtanzania kwa kuviongeza vionjo kwenye hizi kazi mpya ndio kuendeleza kuwepo utamaduni kwa yule mtoto anayezaliwa leo. GLOBALIZATION IS NOT A NORMAL LITTLE WORD. Naomba ZIGO IRUDI PLEASE Mbali na hayo pongezi ziwajie kwa wingi kwa operation ya kupunguza masimu feki
#WeWantZigo

Maoni yako ni yapi mdau????

Related Posts

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.