VODACOM YATOA MSAADA WA SHILINGI MILION 40 KWAAJILI YA WIKI YA USALAMA BARABARANI

Vodacom yapiga jeki wiki ya usalama barabarani

Kampuni ya Mawasiliano  ya Vodacom Tanzania leo imetoa msaada wa shilingi milioni  40 kwa serikali ya Jamhuri ya Tanzania kwa kupitia Baraza la Taifa la  Usalama Barabarani na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika kufanikisha wiki ya usalama barabarani mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo mkoani Arusha.

 

Hafla ya kukabidhi hundi ya fedha hizo imefanyika leo katika wizara ya Mambo ya Ndani ambapo Waziri wa Mambo ya  Ndani ya nchi,Mheshimiwa Mathias Chikawe,alikuwa mgeni rasmi  pia alikuwepo  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu na Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohamed Mpinga.

 

 Akiongea wakati wa halfa hiyo mgeni rasmi,  Waziri  wa mambo ya ndani, Mheshimiwa Chikawe,alisema” Nachukua fursa hii kuwashukuru wadhamini wa kampeni ya usalama barabarani kwa mwaka huu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania  kwa kutoa mchango wao  na kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani kufikia malengo kwa kuhakikisha usalama wa raia na kupunguza ajali za barabarani .
Alisema ajali za barabarani zinaongezeka kwa kasi na kusababisha upotezaji wa nguvu kazi huku zikiacha maafa makubwa kwa taifa, ni jukumu la kila Mtanzania kuwa sehemu ya kusimamia na kuzingatia sheria za barabarani na kuyataka makampuni mengine kuunga mkono jitihada hizi za kupunguza ajali nchini.

 

 Akiongea kwa niaba ya Vodacom Tanzania, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano,Georgia Mutagahywa alisema Vodacom Tanzania inajivunia kuwa sehemu ya juhudi za kuokoa maisha ya watanzania  na mali zao na inayo dhamira ya kuhakikisha inashirikiana na wadau wote wenye wito wa kusaidia usalama barabarani”

“Vodacom Tanzania tumeingia katika kampeni ya kupunguza ajali na madhumuni yetu makubwa ni kusaidia kufanikisha juhudi zinazofanywa na jeshi la polisi kusimamia na kupunguza matokeo ya ajali za barabarani, kila mwaka  kunakuwa na matukio ya ajali za barabarani ambazo zingeweza kuepukika kama wahusika wangekuwa na elimu ya kutosha.Kama kampuni ya mawasiliano tutakuwa mstari wa mbele kuelimisha  jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unaongea na simu ya mkononi”.Alisema Mutagahywa.

Aliongeza kuwa Vodacom imekuwa mstari wa mbele kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii katika sekta ya elimu,afya,kupambana na umaskini na hivi sasa imejikita rasmi katika kampeni za kupunguza ajali nchini na siku zote itakuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha  inahamashisha na kutoa elimu itakayofanikisha kupunguza tatizo la ajali za barabarani

001.WAZIRI

Waziri wa Mambo ya ndani Mathias Chikawe,akipokea hundi yenye thamani ya shilingi Milion 40/=toka kwa Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa(kushoto) msaada huo umetolewa kwaajili ya maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani Mkuu wa jeshi la polisi nchini Ernest Mangu na kulia ni Mkuu wa usalama barabarani Mohamed Mpinga.

004.WAZIRI

Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa(kushoto)   sakiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi msaada wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 40/= kwaajili ya maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani itakayofanyika hivi karibuni jijini Arusha.Katikati ni Waziri wa Mambo ya ndani Mathias Chikawe nakulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mbarak Abdulwakili.

 

Related Posts

Leave a Reply