Wateja 225,000 wa Vodacom wajiunga na huduma ya ujumbe mfupi ya uzazi salama

Asha Othaman (32) hana tena sababu ya kuwa na hofu ya kuhusu kliniki zake za uzazi na tiba ya Malaria inapohitajika kwani yeye na maelfu ya wanawake wajawazito na wazazi hapa nchini sasa wanakisaidizi mikononi mwao kinachowawezesha kupokea taarifa muhimu za afya ya uzazi ikiwemo zinazohusu maendeleo ya ujauzito na kichanga.

Hatua hiyo inafuatia kuzinduliwa kwa huduma mpya ya kujisajili ya Helathy Preganancy, Healthy Baby (HPHB) inayowapa nafasi wanawake wajawazito na jamii kwa ujumla kupokea taarifa mbalimbali muhimu zinazohusu ujauzito ikiwemo kumkumbusha aliyejisajili kuhusu maendeleo ya ujauzito wake na siku za kliniki.

Zaidi ya wateja 225,000 wa Vodacom tayari wameshajiunga na huduma hiyo ya HPHB na tayari wameshapokea ujumbe mfupi zaidi ya 18 Milioni kupitia simu zao za mkononi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es salaam, Ofisa Mkuu wa Mawasisiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Georgia Mutagahywa alisema “ Julai mwaka huu, Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii – Vodacom Foundation iliahidi kuwezesha wateja wake kujiunga na kupokea taarifa husika bila ya malipo kwa angalau kipindi cha mwaka mmoja.”

001.WAZIRI 002.WAZIRI 004.WAZIRI 005.WAZIRI

 Mutagahywa amesema uamuzi huo wa Vodacom umeigharimu Vodacom Foundation Dola za Kimarekani 750,000 (zaidi ya Sh 1,200,000,000/-) hadi kufikia Agosti 31 mwaka huu ambazo ni gharama za taarifa ambazo wateja wa Vodacom wanapokea kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi (sms) kupitia simu za mkononi..

 Mutagahywa amesema Vodacom Foundation kwa kushirikiana na taasisi ya CDC imelenga kufikia mwaka 2016 kuendelea kusaidia kutatua changamoto za afya ya uzazi na malezi ya utotoni hapa nchini. “Vodacom Foundation ina ndoto ya kuona zaidi ya wateja nusu milioni ya wateja wa Vodacom wakijiunga na kunufaika na huduma hii na hatimae kuokoa maisha yao na ya watoto ifikapo mwaka 2016.”Alisema

“Kupata taarifa zenye kuweza kuokoa maisha ya mtu sio jambo la anasa bali ni la lazima na kwamba Vodacom Foundation inajiskia furaha kuwezesha teknolojia ya simu za mkononi ikifanya hivyo.”  

Kwa upande wake Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Suleiman ameipongeza Vodacom Foundation, CDC na wabia wengine kwa kusaidia kampeni za afya ya uzazi na afya ya mtoto hapa nchini.

Waziri Dk. Seif amesema takwimu za hapa nchini zinaonyesha kwamba mwanamke mmoja kati ya 38 hukabiliwa na hatari ya kupoteza maisha kutokana na masuala yanayohusiana na afya ya uzazi huku watoto 48,000 wakipoteza maisha mara tu baada ya kuzaliwa.

Amesema kutokana na hali hiyo, serikali inathamini na kukaribisha kila mchango kutoka sekta binafsi ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo.   

Kiongozi wa Mradi kutoka CDC Saulo Muttah amesema ubia wa Vodacom Foundation na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kugharamia mradi huo wa kuwapatia wanawake na wajawazito taarifa za afya ya uzazi bila ya malipo ni mchango muhimu katika kuimarisha sekta ya afya nchini.

Amesema PEPFAR kupitia Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa cha Serikali ya Marekani (CDC) kimekuwa kikifadhili utekelezaji wa mradi huo kwa ubia.

“Zaidi ya asilimia 50 ya wateja waliojiunga na huduma hii ya HPHB ni wa kampuni ya Vodocom hivyo kwa Vodacom Foundation kufadhili wateja wa kampuni hiyo kupokea taarifa hizo bure ni jambo la msingi na la muhimu kuunga mkono juhudi za serikali za kufikia malengo ya millennia nambari 4, 5 na 6.” Alisema Muttah

Muttah ameonesha matumaini yake kwamba kwa ufadhili wa aina hiyo kutoka kwa makampuni ya simu huduma hiyo itaandikisha watumiaji zaidi ya Milioni Moja ifikapo katikati ya mwaka 2016.

Related Posts

Leave a Reply