WHAT SHOULD I LOOK FOR IN A PARTNER?

What should i look for in a partner?

African American couple outside

Hili swali linawahusu wote.. mnatafuta nini ndani ya wenza wenu, ni kitu gani mnaangalia/mnakiona ndani ya mtu unayeamua kuwa nae kama mchumba/mme/mke. Je, ni macho yake au tabasamu , ama ni sense of humor yake yaani tabia yake, uchangamfu au upole, ni kitu gani unachokiona ndani ya mtu kinachokuvutia. Wengine wanavutiwa jinsi mtu anvyofikiria, au mwili wake, wewe je??

Unaweza ukawa umevutiwa na kitu kimoja wapo, lakini unajua mahusiano mazuri hayajengwi na vitu hivi tu, kuwa na mahusiano mazuri na mwenza wako inahusisha vitu vingi sana tofauti na tabasamu lake .

Iwe unatafuta mtu wa kuwa nae au kama tayari upo katika mahusiano hakikisha mnakubaliana na partner wako vitu vya muhimu mnavyotakiwa kuzingatia katika mahusiano yenu. Sio rahisi kuwa na amani kila saa na kila siku ndani ya mahusiano lakini inawezekana. (Building a healthy relationship)

WHAT SHOULD I LOOK FOR IN A PARTNER

Hivi ni baadhi ya vitu unavyotakiwa kuangalia ndani ya partner wako kama unataka mahusiano mazuri (healthy relationship)

 • Anakupa heshima yako, haijalishi kama yeye ni mkubwa kwako.
 • Anaheshimu maamuzi yako, kama ni katika kazi au kitu unachoamua kufanya na sio kukucheka au kukudharau.
 • Hakuweki chini, anakupa support.
 • Hakasiriki ukispend time na marafiki au familia yako, unatakiwa kuwa na uhuru wa kujichanganya na watu wengine sio yeye tu.
 • Anasikiliza mawazo yako na kukushauri.
 • Mnashare vitu unavyovipenda kama vile kuangalia movie, aina ya music, kucheza. Angalau muwe na kitu kimoja ambacho wote mnapenda ili muwe na kitu cha kufanya pamoja, vitu vingine mnaweza kucompromise tu.
 • Hayupo negative kwa kila kitu, maisha yataenda vipi kama mtu anachukulia kila kitu vibaya.
 • Awe comfortable na marafiki na familia yako.
 • Awe anaheshimu boundaries, sio atake kujua kila kitu chako kama vile kukagua simu au wapi unapokua masaa 24, kama mpo katika mahusiano manatakiwa muweze kuaminiana.
 • Asiogope kukuambia mafeelings yake, hii ni ili muweze kusuluhisha matatizo yenu, na sio kukaa na vinyongo.
 • Anakuhimiza/anakupa moyo uwe na bidii katika kazi au masomo yako.
 • Hakutishi wala kukupiga na kukufanya umuogope.

Kumbuka mahusiano yanahusisha watu wawili, wote wewe na partner wako muwe na usemi ndani ya mahusiano yenu na msiogope kuambiana mnachofeel, na sio kuambiana tu, hata kusikilizana.

Ndani ya kila mahusiano kuna kugombana, na hiki ni kitu cha kawaida kabisa. Wale mnaowaona wana furaha katika mahusiano yao wameweza kujua jinsi ya kuyarekebisha kila mara kitu kibaya kikitokea.

 

Related Posts

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.