Yatima Kituo cha Mwandaliwa wawezeshwa kuanzisha mradi wa kujipatia kipato

Kituo cha Kiislamu cha kulelea watoto yatima na ushauri  cha Mwandaliwa Islamic Orphans Home and Counseling Support (MIOCA’S) kilichopo Mbweni jijini dar es salaam kimepokea Sh 20 Milioni kutoka Vodacom Foundation kusaidia mradi wa ushonaji na ufugaji ili kujijenga kiuchumi.

Fedha hizo zimekabidiwa kituoni hapo wakati na wafanyakazi wa Vodacom waliotembelea kituo hicho kwa lengo la pmaoja na mambo mengine kuwaislisha pia Zawadi mbalimbali walizozikusanya wka ajili ya watoto wanaelelewa kituoni hapo.

Akikabidhi hundi ya fedha hizo kwa niaba ya Vodacom Foundation, mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo Angela Mwakasege amesema Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation wakati wote inaguswa na changamoto zinazoizunguka jamii ikiwemo suala la watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu.

Amesema hatua ya kukabidhi fedha hizo pamoja na zawadi za vitabu na vifaa mbalimbali vya kuchezea watoto ni kielelezo cha jinsi ambavyo wafanyakazi na kampuni kwa ujumla inayoguswa na kusukumwa kusaidia jamii na kuweka mbele ajenda ya kusaidia kukabiliana na changamoto hizo

“Leo tunafuraha sana kufika hapa, tunawapenda sana na tunaimani kwamba hiki tunachpowakabidhi kitawasaidia kutimiza lengo lenu la kujijengea uwezo wa kiuchumi kupitia miradi mnayokusudia kuianzisha ya ushonaji na ufugaji.”Alisema Mwakasege

“Kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Vodacom kipekee tunawpongeza sana walezi na viongozi wa kituo hiki kwa namna mlivyokubali kujitoa kuwalea watoto hao. Sisi tunatambua kuwa hiyo sio kazi rahisi, tunawatia moyo mzidi kujitoa kwa ajili ya akzi hii.”Alisema

Kituo hicho chenye watoto 94 kinatarajia kuanzisha miradi ya ushonaji na ufugaji itakayotumika kukiwezesha kituo kuwa na vyanzo vya mapato na pia kuwa na fursa ya kuwajengea uwezo wa stadi za kazi na kujiajiri watoto ili kuwapa uwezo wa kujitegemea katika siku za usoni.

Kwa sasa kituo hicho kinajiendesha kwa kutegemea misaada ya wahisani mbalimbali, lakini kuanzishwa kwa mradi huo wa ufugaji kuku wa nyama na ushonaji kutawezesha kituo hicho kuounguza utegemezi wa wahisani.

Akisoma maelezo ya kituo na shukrani kwa Vodacom Foundation na wafanyakazi wa Vodacom kw akile walichowawezesha, Katibu wa kituo hicho Omary Ramadhan amesema watoto walio wengi hupatikana kwa kuletwa kupitia Ofisi za Ustawi wa Jamii wilaya ya Kinondoni na husomeshwa na wengi wao wapo katika ngazi mbalimbali za elimu kuanzia ya chekechea.

Akizungumzia msaada huo, xx alisema “ Tunashukuru sana kwa kuitikia wito wetu na baadae kukubalika kwa ombi letu ka kusaidia fedha kufadhili mradi wa ufugaji na ushonaji. Tunajua haikuwa kazi nyepesi, tulihataji kuwa wavumilivu lakini hatiame tuanshukuru sana kuona leo tunaelekea kutimzia ndoto yetu ya kuwa na miradi ya kiuchumi.”

001.MWANDALIWA 002.MWANDALIWA 003.MWANDALIWA 004.MWANDALIWA 005.MWANDALIWA 006.MWANDALIWA 007.MWANDALIWA

Related Posts

Leave a Reply