TBT ::: Zari asema anataka harusi yake na Diamond iwe kubwa na ya gharama kuwahi kutokea Afrika Mashariki

Hii nimeikuta Bongo5 nikasema niweze share hii 

Zari The Bosslady amedai kuwa anataka harusi yake na Diamond Platnumz iwe kubwa na yenye gharama kuwahi kufanyika Afrika Mashariki.

Hata hivyo, itafanyika baada ya kuwa wamefanya mambo ya muhimu zaidi ikiwemo kujijenga zaidi walivyo sasa. Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Alhamis hii, Zari amedai kuwa suala la kufunga ndoa sio kitu kinachowapa pressure. Amedai kuwa hawajawahi kukaa chini na kuwa na majadiliano ya kina kuhusu ndoa, licha ya hadi sasa kuwa na watoto wawili, Tiffah na Nillan. Staa huyo wa Uganda amedai kuwa moja ya mambo ambayo wanataka kufanya ni kuhakikisha kwanza wanawajengea watoto wao apartments zao zitakazowasaidia katika maisha yao hata kama wazazi wao wasipokuwepo. Hata hivyo Zari amedai kuwa mwezi March mwaka huu Diamond ataenda rasmi kujitambulisha kwa baba yake na kuhalalisha uhusiano wao pamoja na kuomba mkono wa ndoa.

Related Posts

1 Comment

  1. All the best.
    Mwanamke kichwa, apartment za watoto!!!

    But harusi yakuvunja record East Africa kuwe hakuna Invitation Cards!!!! Sote tuhudhirie rule tunywe tushereheke!! Cards only kwa VIP na daraja lifuatalo. Lol

    East African Wed

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.